Thursday, April 11, 2013

WAKATI RAGE WA SIMBA AKIJIANDAA KUIPELEKA MAHAKAMANI AZAM FC, CLUB HIYO IMEMJIBU NA KUMWAMBIA KUWA ITAMPATIA HADI NAULI YA KUMFIKISHA MAHAKAMANI

KLABU ya Azam FC imetoa 'Go Ahead' kwa Simba kwenda mahakamani kwa madai ya fidia ya kuchafuliwa.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alikaririwa mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria vikao vya bunge kuwa klabu yake inaandaa barua ya kuidai fidia ya Sh1.5 Bilioni.

Ni kutokana na klabu ya Azam kuwafungia wachezaji wanne kwa tuhuma za kupokea rushwa ambayo ni  Sh7 milioni ili wapange matokeo wakati wa mechi ya Simba na Azam FC Oktoba 26, mwaka jana ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo.

Kauli ya Rage inafuatia taarifa iliyotolewa Jumatatu wiki hii na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) ikieleza kushindwa kuthibitisha tuhuma za kupokea rushwa zilizokuwa ziwawakabili wachezaji wanne wa Azam, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Deogratius Mushi na Said Mourad.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassoro Idrisa alisema kuwa, klabu yake haiwezi kuzuia kusudio la Simba

"Kama Simba inataka kwenda mahakamani ni sawa hatuwezi kuwazuia kwani ni haki ya kila moja isipokuwa ninachoweza kusema tupo tayari tukihitajika.

"Azam ina wanasheria ambao watakwenda kukutana nao kwa ajili ya mapambano ya kisheria na huko ndiko tunakapowasilisha hoja zetu,".alisema Idrisa.

Awali, Rage alisema kuwa tayari ameshawasiliana na mwanasheria wa klabu yake baada ya kupata nakala ya hukumu iliyotolewa na Takukuru alisema kuwa klabu yake imefikia uamuzi huo kutokana na kudhalilishwa kwa muda mrefu tangu uongozi wa Azam ulipotangaza kuwafungia wachezaji hao.
kijiweni bongo by paul koka

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI