Polisi
wa Kituo cha Nandi chini Kenya wanamshikiria mwalimu mkuu wa
shule ya msingi St. Paul kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi
wa darasa la sita na kisha kumlazimisha aitoe....
Kwa
mujibu wa bodi ya shule hiyo, mwalimu huyo amekuwa akifanya
mapenzi na mwanafunzi huyo wakati wenzie wakijisomea darasani
nyakati za usiku katika masomo ya jioni.....
Binti
huyo aliyekumbwa na mkasa wa aibu alikuwa ni kiranja mkuu wa
shule hiyo na inadaiwa kuwa mwalimu mkuu ndiye aliyesimamia
uteuzi wa binti huyo ili aweze kumnasa kiulani.....
Habari
zinadai kuwa baada ya mwalimu huyo kugundua kuwa binti huyo
anamimba, mipango ya kuitoa mimba hiyo ilianza mara moja....
Kwa
mujibu wa mwalimu mmoja wa shule hiyo,Zoezi hilo chafu
lilifanyika katika hospitali ya wilaya ya Kapsabet na kwamba
wakati oparesheni hiyo haramu ikifanyika, walimu wenzake walipata
taarifa kutoka kwa mmoja wa manesi wa hospitali hiyo na
ndipo walipochukua hatua ya kuwajulisha wazazi wa binti huyo
ambao waliamua kwenda polisi.....
kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI