Friday, October 19, 2012

VODACOM IMEKUBALI YANGA KUKATAA JEZI ZENYE NEMBO NYEKUNDU, IMETOA HIZI TATU WACHAGUE ITAKAYOTUMIKA BADALA YA NYEKUNDU

.
Mwandishi wa habari Shaffih Dauda ameandika kwamba kampuni ya simu za mkononi Vodacom ambao pia ni wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wamefikia muafaka na klabu ya Yanga juu ya kutotumia jezi zenye nembo nyekundu.
Vodacom imefikia hatua hiyo kutokana na Yanga kupeleka maombi yao ya kuomba kutotumia nembo hiyo nyekundu katika jezi zao, vodacom imeona ni busara kuwasikiliza Yanga hivyo kuamua kuipa nafasi ya kuchagua nembo moja kati ya hizo tatu hapo juu.
Hii ndio walipewa mwanzo.
Kama wewe ni shabiki wa Yanga, ipi nembo nzuri kati ya hizo tatu?

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI