Friday, October 19, 2012

HIVI UMEISIKIA KAULI YA DR ULIMBOKA? SENTENSI ZAKE NNE PAMOJA NA ALIEMTAJA VIKO HAPA.HIVI UMEISIKIA KAULI YA DR ULIMBOKA? SENTENSI ZAKE NNE PAMOJA NA ALIEMTAJA VIKO HAPA.

Dr Ulimboka aliporudi Tanzania Augost 12 2012.
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu toka arudi Tanzania kutoka kwenye matibabu, hatimae mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari Dr. Steven Ulimboka ameamua kuweka wazi jina la mtu aliempigia simu na kukutana nae muda mfupi kabla ya kutekwa na kuteswa na kisha kutelekezwa kwenye msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Dar es salaam usiku wa july26 2012.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandaliwa na Dr. Ulimboka na kusainiwa na mwanasheria wake Rugemeleza Shayo ambayo imesomwa kwa vyombo vya habari na wakili wake Nyaronyo Kichele, imeeleza kwamba siku aliyotekwa na kuteswa alikua na mawasiliano na afisa usalama aliemtaja kwa jina la RAMADHANI ABEID IGUNDU na kuamplfy zaidi kwamba anashangaa mpaka sasa huyu mtu hajakamatwa wala kuhojiwa.
Dr Ulimboka hospitalini june 29 2012.
Kwenye hiyo taarifa, pia Dr. Ulimboka amesema taarifa zote zilizoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu yeye ni za kweli ambapo amesema yuko tayari kuweka wazi ukweli wote iwapo itaundwa tume huru kushughulikia jambo hilo ili haki itendeke.
Namkariri kwenye taarifa yake akisema “Mimi Ulimboka Steven ni raia wa Tanzania ambae ninafahamu nina haki ya kuishi na kuwa serikali yangu na wananchi wenzangu wanajukumu la kuulinda uhai wangu, wale wote waliotuhumiwa na ninaowatuhumu kunitendea unyama huu wako huru na hakuna aliewagusa, je uhai na maisha yangu yana thamani ndogo kama ya mnyama anaekwenda machinjioni?”- Dr. Ulimboka
Kwenye sentensi ya mwisho namkariri Dr Ulimboka akisema “Je serikali ya nchi yangu itakubali lini kuundwa kwa tume huru kuchunguza unyama huu na kuhakikisha kuwa haki inatendeka? je kuna watu katika nchi yetu ambao wana haki ya kutenda unyama kwakuwa wako juu ya sheria? hiyo sio Tanzania ninayoifahamu, niko tayari kuhojiwa na kutoa ushirikiano wangu kwa vyombo huru na makini vya uchunguzi ambavyo vitaundwa kuubaini ukweli”
Msikilize wakili wa Ulimboka hapo chini….

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI