Friday, October 19, 2012

HALI INAENDELEA VIZURI WATU WAMETOKA MSIKITINI WAKIWA NA AMANI NA WAMEELEKEA MAKWAO

Hali inaonyesha kuendelea kuwa nzuri hadi hivi sasa huko nyumbani Zanzibar, Misikiti mingi imememaliza ibada ya swalah ya Ijumaa na waumini wanaondoka kwa nidhamu kabisa.

Wananchi wametimiza wajibu wao wa kuiskiliza serikali na kwa upande wa serikali ni kutimiza wajibu wao wa kutoa taarifa za Ust Farid na pia kuwafikisha mahakamani wale walioua askari na pia kuwafikisha mbele ya sheria wale WANAOTUHUMIWA KUWA CHANZO cha fujo hizi.

Dr Ali M Shein, Rais wangu, Mzee wangu usikae kimya, ni Imani yangu kuwa utakaponyanyua sauti yako juu ya kadhia hii basi mambo yataleta sura.

Kumbuka kuwa wewe ndio mas'uul juu ya wananchi yako, na kila mchunga ataulizwa kwa kila alichokichunga. Tumesikia msimamo wa serikali yako, lakini majonzi ya wananchi yatapungua zaidi kama watasikia kutoka kwako.

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI