Saturday, October 20, 2012

TASWIRA ZA VURUGU ZANZIBAR BAADA YA KUKAMATWA SHEIKH FARID WA UAMSHO...!!!









Picha kwa hisani ya Team JG Zanzibar
---
Taarifa kutoka mjini Zanzibar  zinasema kuwa hivi sasa Zanzibar kuna vurugu Kubwa zinazoendeshwa na wana uamsho wanaomtafuta kiongozi wao aliyetekwa Jana usiku. Kwa hiyo Eneo la Darajani hapakaliki. 

Habari zilizogaaa kila kona sasa hivi ni kwamba Sheikh Farid wa Uamsho ametekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa hajulikani yuko wapi.

Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.

Hata hivyo, wananchi wa Zanzibar wanasema polisi, UAMSHO na serikali wangesubiri wanafunzi wamalize mitihani ya Form 4 kabla ya wao kuanza malumbano yao! 

Kutokana na Vurugu hizo imerepotiwa kwamba sehemu ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi imechowa moto na imeungua kwa kiasi kikubwa. Mapka sasa hakuna aliyeripotiwa kuumia wala kupoteza maisha katika vurugu zinazoendelea hivi sasa huko zanzibar.

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI