Saturday, October 20, 2012

Matangazo ya kupinga Muungano, yachanwa na kubanduliwa Zanzibar

Matangazo ya kupinga Muungano, yachanwa na kubanduliwa Zanzibar

Matangazo ya kupinga Muungano, yachanwa na kubanduliwa Zanzibar

Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

UONGOZI wa Baraza la Manispaa Zanzibar, (ZMC) jana wameanza zoezi la kubandua matangazo ya kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyobandikwa katika manispaa hiyo.

Matangazo hayo na Vipeperushi yalinza kubandikwa usiku wa kumkia juzi katika nyumba za ibada majengo ya serikali na katika nyumba za watu binafsi katika mitaa mbali mbali ya mji Mkongwe wa Zanzibar.

Vipeperushi  na  mataganzo yameibua mjadala mkubwa Zanzibar kutokana na kuwa na ujumbe mkali dhidi ya Muungano pia yakiwa na picha ya  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein pamoja na Picha za Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikhe Abeid Amani Karume.

Mkurugenzi wa Baraza hilo Rashid Ali Juma, alisema kwamba wameamua kuyabandua matangazo na vipeperushi vya kupinga muungano kutokana na kubandikwa kinyume na sheria.

Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria matangazo ya aina yoyote yanatakiwa kabla ya kubandikwa muhusika kueleweka , yakaguliwe ujumbe wake, yalipiwe na lazima yazingatie mila na Utamaduni na kuepuka kuwa na ujumbe wa uchochezi katika jamii ya Wazanzibari.

Rashid alisema kwamba matangazo ambayo yamebeba ujumbe wa uchochezi kwa mujibu wa sheria hayaruhusiwi kubandikwa katika manispaa ya Zanzibar.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba matangazo hayo na vipeperushi yamekuwa yakibandikwa katika nyumba za ibada, masoko, majengo ya serikali na katika vituo vya umeme kitendo ambacho kinyume na sheria.

Rajab alisema kwamba matangazo na  vipeperushi vya kupinga muungano vimeanza kuonekana  usiku wa kumakia juzi katika Manispaa ya Zanzibar na ZMC inaendelea kuwatafuta watu waliobandika matangazo hayo.

“Tumeamua kuyabandua kwa sababu yamebandikwa kinyume na sheria za nchi”alisema Mkurugenzi huyo.

Afisa matangazo wa Baraza hilo Mwamvua Nassor Salum, alisema kwamba wahusika kabla ya kubandika matangazo hayo walitakiwa kulipia kila matangazo 100 Silingi 100,000 baada matangazo yao kukagukliwa na kulibia maombi yao kwa gharama ya Shilingi  50,000 kabla ya kuruhusiwa kufanyakazi hiyo.

Mwamvua alisema kwa mujibu wa sheria matangazo aina yoyote hutakiwa kukanguliwa na baraza hilo ili kuangalia yamezingatia kwa kiwango gani mila na Utadamaduni pamoja na kuepuka kuwa na ujumbe wa uchochezi ambao unaweza kuvuruga amani na mshikamano.

“Masoko yote yamevamiwa na kubandikwa matangazo ya kupinga muungamno wetu leo tumeanza kazi ya kubandua katika soko la darajani na Mwanakwerekwe.”alisema Mwamvua.

Alisema kwamba baada ya kubandua matangazo hayo watabandika matangazo ya onyo kwab watua kuacha kubandika matangazo au vipeperushi bila ya kufuata taratibu za kisheria.

Vipeperushi na matangazo hayo yamekuwa yakisabazwa na Waziri asiyekuwa na Wizara maalum Mansoor Yussuf  Himid, yakiwa yamefungwa katika mabunda yakiwataka wananchi kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mapema juzi majira ya  saa 6:15 mchana Waziri Mansoor alionekana akipakuwa mzigo wa mabunda ya vipeperushi na matangazo na kuweka katika vikapu vya wachuuzi  kutoka katika  gari aina ya Tayota Z 707 AK na kuwakabidhi wachukuzi huko katika Soko Kuu la darajani Zanzibar.

 “Wewe uwezi kupata mambo haya yanakwenda kwa watu maalum”alisema Mansoor ambaye pia Mujumbe wa halimashauri kuu ya CCM.

Matanagazo hayo na vipeperushi vinasema “Kudai Utaifa wa Zanzibar ndiyo dhamira ya Mapinduzi ya 1964” walipindua wazanzibari Tujitawale”  “Usiseme Muungano sema wa mkataba Tuu”  “Tuacheni Tupumue” yanasomeka huku wanamapinduzi wakiwa katika Picha ya pamoja akiwemo Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikhe Abeid Amani Karume.

 “Maoni ya Wazanzibari kutaka Muungamno wa mkataba yaheshimiwe”  matangazo hayo yanasomeka huku Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein, akionekana katika Picha akihutubia wanachama wa CCM ” Kataa Malaria, Kataa Ukimwi, kataa muungano wa Serikali mbili’ vinaogeza Vipeperushi hivyo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema kwamba  CCM haihusiki na matangazo hayo ya kupinga muungano wa Tanganyika Zanzibar.

Alisema kwamba CCM imesikitishwa na watu walioamua kuchukua picha za waasisi wa Mapinduzi na viongozi wa serikali na kutumia kutengeneza ujumbe wa kupinga muungano wa Tanganyika Zanzibar.

Hata hivyo alisema kwamba CCM tayali imechukua hatua ikiwemo kuvitarifu vyombo vya dola kutokan na picha hizo kutumika kwa vitendo vya uchochezi ambavyon vinaweza kuvuruga amani na mshikamano kwa wananchi wa Zanzibar.

Alisema kwamba kama kuna Viongozi  wanapinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar walitakiwa kutumia vikao au Tume ya  mabadiliko ya katiba kutoa maoni yao badala ya kuwasemea uhogo viongozi waliotangulia mbele ya haki Zanzibar.

“Matangazo hayo na  vipeperushi sio ya CCM na tuna laani vikali kitendo hicho.”alisema Vuai.

Hata hivyo baadhi ya wananchi katika manispaa ya Zanzibar wamekuwa wakiwekewa vipeperushi vya kupinga Muungano katika vikapu wakiwa katika mahitaji ya huduma katika soko la Mwanakwerekwe na soko Kuu la darajani Zanzibar.

Akizungumza na Nipashe mjini Zanzibar kamishna wa Jeshi la Polisi Mussa Ali Mussa, alisema kwamba hadi jana alikuwa bado hajapokea taarifa yoyote kuhusu tukio hilo kutoka kwa makamanda wake

Matangazo hayo yameibuka huku Jumuiya ya Uamsho na Mihahadhara ikiendelea na kampeni zake msikitini za kutaka Zanzibar kujitenga katika muungano na kusababisha
kutokea vurugu na makanisa na baa kuchomwa moto Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI