Saturday, October 20, 2012

NEWS ALERT: HALI SI SHWARI KARIAKOO, VURUGU KATI YA POLISI NA WAISLAMU ZAENDELEA...!!! "TUKISHA POTEZA AMANI NI VIGUMU SANA KUIRUDISHA."







Inasemekeana Police wanazuia maandamano ya waislamu huko Kariakoo jijini Dar. (Picha hii kwenda juu ni kwa hisani ya  Andrew Chale)
Pichani ni Vipeperushi  vilivyotolewa na Waumini wa Dini ya Kiislamu kabla ya maandamano leo. (Picha kwa hisani ya Mo Blog)

Waandamanaji wakionekana kabla ya vurugu kuanza
Msimbazi Kariakoo hali ya mabomu na risasi zimetumika kutawanya watu wanao taka kuandamana. Magari ya polisi takribani matano yako eneo la tukio kuhakikisha kuna hali ya usalama. Maduka mengi sana yamefungwa kwa hofu. Magari yanayo ingia nakutoka pia yamepungua sana.
Pichani ni Jeshi la Wananchi Tanzania likiwasilia maeneo ya Kariakoo kuongezea nguvu kwa ajili ya kutuliza ghasia.
Inasikitisha sana
Hii ni Kariakoo mda mchache uliopita 
Wanajeshi wamemwagwa (Thanks James for the pic)
Kikazi zaidi! Fanya Fujo Uone

UPDATE YA VURUGU ZA LEO: Kamanda wa Polisi Suleiman Kova amezungumz muda mfupi uliyo pita kupita Clouds Fm na kusema kwamba hali kwa sasa ni shwari.
---
HALI ya jiji la Dar es Salaam imeweza kuwa tete kwa muda wa masaa kadhaa kufuatia baadhi ya wanaodaiwa kuwa waumini wa taasisi za dini za kiislamu kushinikiza kuandamana kwenda Ikulu kudai haki mbalimbali hapa nchini ikiwemo kushinikiza kuachiwa huru Shehe Ponda wa taasisi hizo.

Hali tete hiyo ilianza majira ya mchana mara baada ya ibada ya waumini hao wakitoka msikitini na ndipo vurugu ilipoanza hasa katika msikiti wa Kwamtoro uliopp Kariakoo.

Hata hivyo awali, waumini wao kwa wao walitofautiana na muda mfupi Polisi ilipofika hali ilikuwa tete na kuwa uwanja wa mapambano baada ya kundi la watu linalosadikiwa kuwa ni la Kiislamu kusababisha vurugu baina yao na askari polisi katika eneo la Kariakoo.

Vurugu hizo zimekuja kufuatia kundi hilo la waislamu lilipokuwa likikaidi agizo la polisi la kutojihusisha na maandamano, yaliyoanzia katika Msikiti wa Kwamtoro kutaka kuelekea Ikulu, ndipo ilipoanza tafrani hiyo, ambapo vikosi vya polisi wa kutuliza ghasia (FFU)waliwatawanya kwa maji ya kuwasha sambamba na mabomu ya machozi.

Tanzania Daima lilishuhudia tukio hilo ambalo lilizua tafrani kubwa iliyopelekea wasiwasi mkubwa kwa wananchi hususani wafanyabiashara wa eneo hilo, ambao walilazimika kusitisha shughuli zao kuhofia usalama wao.

Aidha,baada ya askari polisi kuonekana kuzidiwa nguvu na waandamaji hao, kutokana kurushiwa mawe, ndipo Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lililokuwa na magari yapatayo 10 yaliyojaa askari wakiwa na silaha kuingilia kati ili kunusuru hali hiyo.

Kwa upande wa waandamaji hao walisikika wakisema kuwa,lengo lao ni kufikisha malalamiko yao kwa Rais Jakaya Kikwete,ili yatafutiwe ufumbuzi wa haraka.

“Hapatakuwa na amani, labda tuonane na Mkuu wa nchi, polisi wakifanikiwa kutuzuia leo ‘jana’ lazima ijumaa ijayo Oktoba 26 tuandamane kama dhamira yetu tulivyokusudia” alisema Juma Othuman.

Wafanyabiashara wanazungumziaje

Wakati vurugu hizo zikiendelea, liliibuka kundi la wafanyabiashara katika eneo hilo likilaani kitendo hicho kinachofanywa na kundi la waislamu kuwa ni cha kikatili kwa sababu, mbali na kuondoa amani ya nchi lakini kinapandikiza chuki baina ya wakristo na waislamu.

“Tunaelezwa kuwa Tanzania ni nchi ya amani, hakuna amani nakataa kwa haya tunayoyaona na kuyashuhudia amani imetoweka, mimi dada unavyoniona ni muislamu halisi lakini nina wasiwasi na hali ya nchi inavyoelekea” alisema Fadhili Mohameid.

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI