NAIBU waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw.Adam Malima amesema kuwa sababu
kubwa ambayo inayochangia kupoteza viti vya ubunge katika maeneo
mbalimbali nchini ni kutokana na makundi yaliyogawanyika ndani ya chama
kipindi cha kura za maoni ndani ya chama hicho.
Amesema kuwa
makosa ambayo huwa yanafanyika wakati wa kupitisha majina ambapo jina
linalopitishwa linakuwa sio chaguo la wanachama hivyo hulazimika kumpa
mtu yeyote kutokana na chama kuweka jina ambalo halitakiwi kwa
wanachama.
Bw. Malima
alisema yote inatokana na chama cha mapinduzi kupoteza viti vya ubunge
katika maeneo mbali mbali ni kutokana wagombea walio wengi kukataliwa
kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho.
Akitolea
mfano Mkoa wa Iringa alisema kwamba Mbunge wa sasa Mchungaji Msigwa hana
uwezo wa kuwa Mbunge katika jimbo la Iringa bali wananchi walilazimika
kumchagua kutokana na kura za maoni ndani ya ccm katika kumchakato wa
kumchagua mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo..
Bw. Malima
alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa
chama cha mapinduzi uliofanyika katika viwanja vya sokoine Jijini hapa.
“Mfano tosha
tunao kutoka Mkoa wa Iringa jina lililopitishwa ndani ya halmashauri
kuu ya CCM halikuwa chaguo la wanachama hivyo wananchi wote
wakalazimika kumchagua Mbunge ambaye hakupaswa kuwa mbunge “alisema Bw.
malima.
Akizungumzia
kwa Mkoa wa Mbeya alisema kuwa kwamba kwa kawaida Mbeya ni ya chama cha
mapinduzi lakini katika uchaguzi uliopita walijikwaa ndio maana ilifika
mahala wakapoteza viti viwili vya ubunge ambavyo ni Mbeya Mjini na
Mbozi Magharibi.
Alisema kuwa
hata Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bw.Mbilinyi nae hana uwezo wa
kuingia bungeni na kuwatetea wananchi wake hali kadhalika na Mbozi
magharibi pia hawafanani na wananchi wanaowaongoza ambao wanatakiwa
kwenda kuwatetea bungeni bali yote hiyo ilitokana na kujikwaa kwa chama .
Hata hivyo
alisema kwamba katika chaguzi mbali mbali ndani ya chama cha mapinduzi
ni sawa na usajili wa timu ambayo itakayokwenda kushindana mwaka 2015
hivyo makosa yaliyofanyika kipindi kilichopita inatakiwa kuyarekebisha
sasa ili kuondokana na makundi yasiyokuwa na tija ndani ya chama cha
mapinduzi ambayo yamekuwa yakitoa nafasi ya kushinda kwa vyama vya
upinzani .
“Uchaguzi
huu ambao tunafanya leo ni usajili wa timu itakayokwenda kushindana
kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 hivyo ni vema tukawa na timu nzuri ambayo
itakuwa na nguvu kubwa na upinzani kushindwa kutumia mianya hiyo ambayo
imekuwa ikitoa nafasi kubwa kwa wapinzani kupenye kwa kutumia makundi
yetu ndani ya chama”alisema Malima.
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI