Wissan al-Hassan. 
Afisa mashuhuri wa kijasusi nchini Lebanon anayeupinga utawala wa Rais Bashar al – Assad, ameuawa katika mlipuko mkubwa wa bomu la kutegwa ndani ya gari katika mji mkuu Beirut.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni dalili nyingine inayoonyesha kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vinaiingiza tena  nchi ya Lebanon katika mgogoro huo.
Kiongozi huyo Wissan al-Hassan ambaye aliongoza uchunguzi uliozihusisha Syria na kundi la Hezbollah katika mauwaji ya Waziri Mkuu wa zamani Rafik al-Hariri, na watu wengine saba waliuawa wakati bomu liliporipuka katikati ya mji wa Beirut.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ki Ban Moon na Waziri wa Mambo ya Nje wa MarekaniBi. Hillary Clinton ni miongoni mwa waliolaani shambulizi hilo.