John
Terry, baada ya kuamua kwamba hana nia ya kukata rufaa kwa kutumia lugha
ya ubaguzi dhidi ya Anton Ferdinand, na kupigwa marufuku asicheze mechi
nne na vile vile kutozwa faini ya pauni 220,000, ameomba msamaha.
Nahodha huyo wa Chelsea, atazikosa mechi nne katika ratiba ya ligi kuu ya Premier.
"Nataka kuomba radhi kwa lugha niliyoitumia katika mchezo huo."
Tume huru
ya chama cha soka cha England, FA, ambayo ilikuwa ikichunguza madai
hayo, iliamua Terry alifanya kosa la kutumia lugha ya ubaguzi wa rangi
dhidi ya mlinzi wa klabu ya QPR, Anton Ferdinand, katika mechi
iliyochezwa uwanja wa barabara ya Loftus, tarehe 23 Oktoba, mwaka 2011.
Terry ameadhibiwa na klabu ya Chelsea.
Hata hivyo, hatua hizo za adhabu zimehifadhiwa kama siri na klabu ya Chelsea.
Katika taarifa, klabu kimeelezea: "John Terry amefanya uamuzi unaofaa wa kuamua kutokata rufaa kuhusiana na uamuzi wa FA.
"Chelsea
pia inatambua, na kuunga mkono hatua hiyo ya John kuomba radhi
kikamilifu kwa lugha aliyoitumia. Klabu kinaamini lugha kama hiyo kamwe
haikubaliki, na ilikuwa ni kinyume na matazamio ya mchezaji mwenye hadhi
na viwango vya John kama mchezaji wa Chelsea."
Wakati
huohuo, mchezaji mwenzake katika timu ya Chelsea, Ashley Cole, ametozwa
faini ya pauni 90,000 kwa kuandika maneno yasiyofaa katika mtandao wa
kijamii wa Twitter, katika kutofurahishwa na hatua ya chama cha FA,
kuhusiana na kesi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Terry.
Mchezaji
huyo wa Chelsea na vile vile timu ya taifa ya England, na mwenye umri wa
miaka 31, alikiri kosa ambalo limetajwa na FA, la kuandika maneno
yasiyofaa, na kuuletea sifa mbaya mchezo wa soka.
Cole, mara baada ya kuandika maneno hayo, aliyafuta, na kuomba msamaha.
Aliepuka
adhabu ya kukatazwa kutoshiriki katika mechi, kwa kuomba msamaha, moja
kwa moja kwa mwenyekiti wa chama cha FA, David Bernstein.
"Alionyesha kwa dhati kujuta hayo," alieleza Bernstein.
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI