Akiongea kwa uchungu , Spika wa Bunge bi Anne Makinda amewashambulia wabunge leo asubuhi na kuwaambia suti zao walizovaa haziendani na matusi yanatoka katika vinywa vyao ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana kwa madai kuwa mdomo wake hauwezi kutamka matusi hayo.....
Makinda amesema matusi ndiyo yamekuwa yakitawala
katika midomo ya wawakilishi hao na kuacha hoja inayojadiliwa hewani....
Spika wa bunge amekwenda mbali zaidi na kuwaambia wabunge hao kwamba hataangalia
chama endapo mbunge atavunja kanuni za bunge kwa kuwa kanuni za bunge
zinampa nafasi ya kuita polisi na kuja kumchukua mbunge huyo kwa hatua
za kisheria.
Makinda amesema
ametumiwa sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake
kuangalia bunge labda ajifungie chumbani.
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI