Tuesday, April 16, 2013

BOB JUNIOR AINGIZWA MKENGE....LAWAMA ZATUPWA TIGO


Imebainika kuwa kuna mtu aliyetengeneza line mpya kwa kutumia namba ya Bob Junior aliye barani Ulaya kwa sasa na kutaka kuwatapeli watu wake wa karibu kuwa yupo hoi na anahitaji msaada haraka.



Taarifa hiyo imetolewa na baba yake mdogo, Guru Ramadhan ambaye ni mmiliki wa G Records. Kupitia Facebook, Guru aka G Lover ameandika:

“Hii sijaipenda kabisa ni too much sasa..eti mtu yupo Europe na simu yake inaita bongo ukipiga duh kumbe mtu katengeneza line mpya na kutumia namba ya Bob Junior na pia jamaa anayetumia hiyo line ya simu eti anaomba msaada kwa watu kuwa Bob Junior anaumwa sana Ulaya anahitaji msaada wako ili arudi Bongo.

Hivi nini maana ya kusajili namba?…makampuni ya simu ya Bongo mjipange sanaaa…hili limemkuta msanii Bob Junior siku chache hizi, mpaka imeripotiwa polisi eti ndio wamejidai kui block number…t.g. mmeniboaje?..so guyz mnaosafiri muwe makini sana mkisafiri maana mnaweza kukuta madeni kibao mkafa na presha bure…wizi mtupu…I hate dat.”
kijiweni bongo by paul koka

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI