kijiweni bongo by paul koka
Leo
asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi
kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni
kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano
kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika.
Mh
Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu jambo hilo uamuzi
wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge
kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale
itakapotokea tukio kama hilo.
Kwa
uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo
ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na
Jumatano wiki ijayo.
Uamuzi
wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu na wengine
watano na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge
umebarikiwa na Mheshimiwa Spika..
Hivyo
Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo
Na adhabu iliyotolewa.
Taswira
ya vurugu zilizotokea bungeni dodoma juzi
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI