Mbunge
wa Maswa Magharibi, John Shibuda anatarajia kuongoza maandamano
makubwa ya ng’ombe kutoka Lusumo Nyakabanga Mkoani Kagera, hadi Ikulu
kwa Rais Jakaya Kikwete ili kupinga uonevu na manyanyaso wanayofanyiwa
wafugaji.
“Kama
watu wanasema ni porojo za Shibuda, basi wasubiri kama hotuba ya
Waziri Mkuu haitakuwa na majibu kwa wafugaji, lazima hayo yatatokea kwa
mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, hawa nao ni binadamu
waambiwe basi kama hawatakiwi Tanzania,” alisisitiza.
Mbunge
huyo alitoa kauli hiyo juzi akiwa na uongozi wa wafugaji kutoka Kanda
ya Ziwa ambao wako Dodoma kwa lengo la kuonana na Mawaziri wa Maliasili
na Mawaziri wa Mifugo akiwemo Waziri Mkuu, ili kufikisha kilio cha
wafugaji ambao wanateketezewa mifugo yao na askari wa wanyama pori.
Shibuda
alisema kuwa “Katika nchi yoyote duniani hakuna mateso yanayofanywa
kwa wananchi wake kama ambavyo inafanyika Tanzania kwa upande wa
wafugaji, ni heri ya wakimbizi watakuwa na amani kuliko hawa
wanaonekana kama takataka.”
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI