Chanzo cha umaskini wa wananchi husika husababishwa na bunge bovu na legelege ambalo kimsingi haliwezi kusimamia serikali.
Kwa sasa
bunge letu limekuwa comedy show bila kujali pesa za
walipa kodi wanazozitafuna kila siku.
Tangu bunge lianze mheshimiwa spika kwa makusudi
amekuwa akiruhusu mijadala isiyokuwa na tija bungeni na wabunge wamekuwa wakitukanana matusi ya
nguoni
Wakati leo nasikiliza bunge,
Mheshimiwa mmoja alisimama tena kwa kujiamini na kudai kuwa
eti umasikini wa tanzania unasababishwa na picha ya nyoka
iliyoko katika pesa zetu....
"Tanzania ni nchi masikini kwasababu tumeweka picha ya nyoka kwenye hela
zetu".... ni kauli ya Mh Livingstone Lusinde Mbunge wa Mtera leo
bungeni.
Kauli aliyoitoa Mheshimiwa Bungeni leo
haiingii akilini hata kidogo. Labda pengine kwa sababu ya upeo
wangu mdogo wa kuelewa na kufikiri .....
Ni vigumu sana kuwashawishi wananchi na jumuia za kimataifa kuwa umasikini na matatizo yote yanayoikabili
shillingi ya Tanzania yanasababishwa na picha za nyoka...
Baadhi ya COMEDY toka bungeni:
-Kianzishwe chuo cha kufundisha wanaume namna ya kuwafundisha namna ya kutongoza wanawake - Mbunge viti maalum Chadema!
-Tanzania ni nchi masikini kwasababu tumeweka picha ya nyoka kwenye hela zetu".. hii ni kauli ya Mh Livingstone Lusinde Mbunge wa Mtera
-Ofisi ya Waziri Mkuu, imeomba Shilingi bilioni moja kwa ajili ya
kuwazika viongozi wa kitaifa watakaokufa katika mwaka wa fedha unaoanza
Juni, mwaka huu.
-Bangi ihalalishwe na kua zao la Taifa!
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI