kijiweni bongo by paul koka
Msanii wa Kundi la Tip Top Connection, Madee au Rais wa Manzese ameeleza kuwa wimbo wake wa Nani Kamwaga Pombe Yangu umempa heshima kubwa.
Msanii wa Kundi la Tip Top Connection, Madee au Rais wa Manzese ameeleza kuwa wimbo wake wa Nani Kamwaga Pombe Yangu umempa heshima kubwa.
Akiongea na mwandishi wetu, Madee, ambaye jina lake halisi ni Hamad Ally
Seneda alisema licha ya kupata shoo nyingi, lakini pia ni wimbo ambao
unapigwa sana kwenye klabu mbalimbali na kila unapopigwa hakuna anayekaa
kitini.
Alisema kuwa kufuatia kutoa wimbo huo ameshakusanya Shilingi 16 milioni.
Alisema pamoja na kupata fedha nyingi kupitia
wimbo huo bado hajaamua azifanyie nini ila ameamua atulie kwanza
akitafakari nini kinafuata.
“Wimbo bado upo juu na unafanya vizuri, hivyo
ninachofanya kwa sasa ni kuendelea kukusanya fedha kutokana na shoo
ambazo nitapata kutoka kwenye wimbo huo baada ya hapo ndio nitajua
nifanyie nini,” alieleza.
Aidha, Madee alisema kuwa anafurahi kuona amefanya
kitu ambacho kila mpenda burudani kinamfurahisha kwani sio wasanii
wengi ambao wanaweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa wale waliopo
kwenye usanii kwa muda mrefu. Kalunde Jamal
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI