Wednesday, April 24, 2013

JAMAA AFUKUZWA KAZI SIKU YA KWANZA TU BAADA YA "KUTEMA MATUSI" OFISINI

kijiweni bongo by paul koka

 Imeandikwa na Subi---wavuti.com
---------
Kuna maeneo ya kazi ambapo utawala una "zero tolerance" kwa aina yoyote ile ya matumizi ya maneno ya kutusi, kukera, kuudhi... yanapotamkwa mbele ya kadamnasi.

Ndivyo ilivyokuwa kwa A. J Clemente, aliyekuwa ndiyo anaanza kazi siku ya kwanza kabisa baada ya kuajiriwa kama mfanyakazi mpya kwa vipindi vya mwisho wa wiki katika chaneli ya KFYRTV ya NBC, Bismark, N.D.


A.J Clemente alitamka maneno "f***ing s**t" bila kufahamu kuwa kamera ilikuwa tayari hewani (LIVE On Air).


Kilichomponza kutamka maneno hayo, ni hasira ya kushindwa kutamka jina la mshindi wa mbio za Marathoni za London,  Tsegaye Kebede. Baada ya kujitahidi kutamka na kurudia na kurudia tena na tena, akajikuta ameshatusi.


Msikilize kwenye sekunde ya 17 katika video iliyopachikwa hapo.


Kila siku twajifunza!



 Imeandikwa na Subi---wavuti.com

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI