Biahara
zote zilisimama kwa muda katika stendi kuu ya mabasi ya Bomet
nchini kenya wikiendi hii baada ya kundi kubwa la wanaume
kumvamia mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa kingua kifupi na kisha
kumvua huku wengine wakimchezea nyeti zake.....
Mwanamke
huyo ambaye inadaiwa alienda katika stendi hiyo kufanya booking
ya basi,alikutwa na kisanga hicho baada ya kuvamiwa na kundi
kubwa la wapiga debe na vibaka ambao walianza kwa kumzomea na
kumrushia makopo ya maji......
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,sakata hilo lilichukua
takribani dakika 15 za kumzomea na kumtukana wakiwa
wamemzunguka kabla ya kumvua nguo zake.....
"Walimzomea
na kumtukana vibaya huku wakiwa wamemzingira.Juhudi za wanawake
wasamaria wema kumuokoa zilikwama kwa kuwa kundi lilikuwa kubwa
na wao walikuwa wanaogopa kufanyiwa hivyo"...Alisema shuhuda huyo
Mbali
na shuhuda huyo,Bwana Sang naye analielezea tukio hilo kwa
kudai kuwa ile sketi ilikuwa ni zaidi ya fupi na pia ilikuwa
nyepesi na ndani ndani hakuwa na kitu, hali iliyosababisha
wapiga debe hao wamvae na kumvua.....
Bwana
Sang anadai kuwa kesi nyingi za ubakaji zimekuwa
zikisababishwa na wanawake wenyewe kutokana na mavazi yao
wanayoyavaa....
Baada
ya tukio hilo kupamba moto, polisi walifika japo walichelewa
na hatimaye kufanikiwa kumwokea mrembo huo mikononi mwa vibaka
hao....
Kutokana
na tukio hilo,shirika la maendeleo ya wanawake limelaani
vibaya tukio hilo na kuahidi kuchukua hatua kali zaidi endapo
udhalilishaji huo utaendelea na kufumbiwa macho....
kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI