Wabunge watano wa Chadema jana walitimuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano kutokana na vurugu zilizotokea jana usiku.
Wabunge hao ni Lissu, Hezekiah Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia
(Ilemela), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless Lema (Arusha Mjini) na
Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Chanzo za kufukuzwa kwao ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu
ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya
kuingilia hotuba ya Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba.
Kutokana na tafrani hiyo, Nchemba hakuweza kuhitimisha hotuba yake
hivyo Ndugai alilazimika kukatisha mkutano wa Bunge.
Hata hivyo wakati
akiahirisha mkutano huo, tayari wabunge hao walikuwa wameshatolewa nje
baada ya askari kuongezwa .
kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI