Askari
mmoja mwanaume anadaiwa kutekwa kisha kudhalilishwa kijinsia na
wanawake wanne kwa karibu wiki moja kabla ya kupigwa mawe na kutupwa
katikati ya milima.
Mateso ya muathirika huyo mwenye miaka 25 yalianza pale alipopata lifti ya gari kuelekea mji wa Mutare nchini Zimbabwe.
Wanawake
wawili na mwanaume mmoja walikuwa kwenye gari, Mercedes Benz, na, baada
ya kuendesha kwa takribani saa moja kuelekea mji huo, dereva wa gari
hilo akabadili mwelekeo wa safari hiyo.
Ndipo muathirika huyo akalalamika, alitishiwa kwa kisu.
Msemaji wa polisi wa Manicaland, Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula.
Msemaji wa polisi wa Manicaland, Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula.
"Askari
huyo alitaka kushushwa, lakini dereva huyo akatoa kisu na kumtishia
nacho. Mmoja wa abiria wanawake akamfunga kwa kitambaa cheusi machoni
mtuhumiwa huyo."
Kwa mujibu wa Nuzondiwa,watesi hao walimpeleka
mlalamikaji kwenye nyumba isiyojulikana ambako walimvua nguo zote na
kumpora simu yake na Dola za marekani 35.
Watuhumiwa walimwamuru mtu huyo kulala na mmoja wa wanawake hao katika matukio kadhaa na alishikiliwa kati ya Aprili 19-23.
Kisha
akafungwa tena kitambaa machoni na kushushwa kwenye Milima ya
Dangamvura ambako, kwa mujibu wa polisi, alipigwa mawe katika mguu wake
wa kushoto, na kumsababishia majeraha makubwa.
Watuhumiwa hao kisha wakawasha gari lao na kutokomea kusikojulikana.Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Sakubva
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI