Thursday, December 27, 2012

SAMATA AWAANGUKIA MASHABIKI STARS


Calvin Kiwia
KATIKA kuonyesha kusikitishwa na mtazamo wa mashabiki
dhidi yake baada ya kushindwa kuichezea Timu ya Taifa (Taifa Stars) mchezo wa kirafiki dhidi ya Zambia, Mbwana Samatta amewaangukia tena mashabiki.

Samata amesema mbali na kutopata fursa ya kuichezea Stars, lakini pia amesikitishwa na mtazamo mbaya ulioonyeshwa na mashabiki dhidi yake.
�Napenda kuwaambia mashabiki kwamba, wasinihukumu kwa kushindwa kucheza, hali yangu kiafya haikuwa nzuri kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya bega,� alisema Samata.

�Nawaomba radhi mashabiki wote Tanzania. Nilishindwa kucheza mechi hiyo kwa sababu ya maumivu ya bega na sikuwa na sababu nyingine yoyote,� aliongeza.

Kocha Kim Poulsen aliwaita Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la kulipwa na klabu ya TP Mazembe ya DRC kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika wikiendi iliyopita.
Hata hivyo wachezaji hao hawakujiunga mapema na wenzao kambini na baada ya kufanya hivyo walidai kuwa wanaumwa, jambo lililowafungulia chuki mashabiki wa soka.

Wakiwa uwanjani kushuhudia mchezo huo ambao Stars ilishinda bao 1-0, Samata na Ulimwengu walijikuta kwenye wakati mgumu wa kuzomewa na mashabiki.

Kupitia ukurasa wake kwenye tovuti ya Facebook, Samata alisisitiza: �Hakuna binadamu aliyekamilika duniani.
Kwa moyo mkunjufu nakubali nimefanya makosa. Naomba radhi kwa Watanzania wote.�

Samata aliyewahi kuzichezea pia timu za African Lyon na Simba kabla ya kutua mazembe, aliandika zaidi: �
�Naahidi hali hiyo haitajitokeza tena. Tunakaribia mwaka 2013 nahitaji radhi zenu.�

Hata hivyo, baadhi ya wadau wa soka walitoa maoni kufuatia ujumbe huo, Mtangazaji wa Shirika la Habari la Uingereza BBC, Erick Nampesya aliandika: �Basi kijana.

Pumzika nadhani imetosha tatizo sasa unatuchanganya.
Umeomba msamaha kwenye gazeti (Mwanaspoti). Ukisema
unaumwa na kwa maana hiyo, unalaumu wanaokutuhumu.�
Anaendelea: �Kuwa na msimamo kijana. Ukweli ni upi hapa?, kama unaumwa hustahili lawama. Msamaha umeomba wa nini wakati wewe ni mgonjwa.� alihoji.

Naye David Zakaria aliandika kwa kusema: �Tanzania ndicho tulichokuwa tukikihitaji kutoka kwako, baada ya kutukosea. Hakika, tunaamini hutorudia tena.� �Pia, elewa Watanzania wanakupenda na kukutakia
mafanikio mazuri. Jaribu kuijali nchi yako.� alisisitiza

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI