Monday, October 22, 2012

WEMA ISSAC ABRAHAMU SEPETU TENAA!!!!!!!!




Na Imelda Mtema
KATIKA kuonesha jeuri ya fedha, Wema Isaac Sepetu amefanya kufuru kama kawaida yake baada ya kumlowanisha mwili mzima kwa pombe za bei mbaya mrembo aitwaye Rehema Kimbu.

Mrembo Wema Sepetu akimwogesha Rehema Kimbu kwa pombe.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri nyumbani kwa mwigizaji Aunt Ezekiel, Mwananyamala, Dar, Ijumaa iliyopita ambapo Wema na Aunt walimfanyia ‘sapraizi’ ya ‘bethidei’ Rehema ambaye ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.
Rehema Kimbu akizidi kumwagiwa kilevi wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa.
Katika hali ya kushangaza, Rehema ambaye ni shosti mkubwa wa Aunt alishtukia anamwagiwa pombe mfululizo aina ya Gordon’s na Jack Daniels huku mwigizaji Nice Chande akimmiminia chupa kubwa kadhaa za maji.
Rehema Kimbu akiwa kalowa mwili mzima baada ya kumwagiwa pombe na Wema (kushoto).
Muda mwingi Wema alikuwa akimmwagia Rehema pombe bila kushusha mkono.
Kufuatia kitendo hicho kilichoambatana na kelele nyingi za mastaa hao,  kilisababisha wapita njia kujazana getini kwa Aunt bila kujua kilichokuwa kikiendelea na kudhani Rehema alikuwa akipokea kipigo.

Vicheko: Rehema akiangua kicheko baada ya sherehe yake kunoga

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI