Monday, October 22, 2012

Wabunge wa Chadema waigwaya keki ya Birthday ya Shy-Rose


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi waliangua Vicheko pale wenzao wa CHAMADA walipoikwepa kuigusa nakuila Keki ya Birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy Rose Banji wakati wa tafrija yake iliyofanyika Nyumbani Longe Jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wa CHADEMA  ni Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Kiwelu picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu.
 
Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.

Huku Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Halima Mdee aongoze Ukataji wa Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby Girl Shy Rose kuliwa, ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.
 
Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge, wanasiasa, Wasanii musiki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake.
HABARI KWA HISANI YA paulkoka5.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI