Karibuni ndugu wasomaji wapenzi katika
blogu hii, ambayo itakuwa maalumu kwa habari za michezo na burudani
pamoja na makala zinazowahusu wasanii na wanamichezo mbalimbali. Na pale
itakapobidi, blogu hii pia itakuwa ikiwaletea habari mbalimbali kuhusu
jamii na matukio ya kimataifa. Karibuni sana kwa kuchangia habari,
makala na mada mbalimbali. Unaweza kuwasiliana nami kupitia email:
ramoza1967@live.com au rashidzahor@hotmail.com au simu namba
0788-455808, 0719-153800.
Sunday, August 5, 2012
SIMBA YASISITIZA YONDANI NI MALI YAO, YATAKA ILIPWE MIL 50/-
Mwenyekiti
wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amesisitiza kuwa, beki Kelvin
Yondan aliyesajiliwa na klabu ya Yanga msimu huu bado ni mchezaji wao
halali.
Rage amesema hayo leo wakati wa mkutano mkuu wa
wanachama wa Simba uliofanyika kwenye ukumbi wa bwalo la maofisa wa
polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam.
Rage alisema Yanga
imemsajili beki huyo kinyume na kanuni kwa vile alishatia saini
makubaliano ya kuongeza mkataba wake na Simba.
Alisema
iwapo Yanga inamtaka mchezaji huyo, inapaswa kuilipa Simba shilingi
milioni 50, vinginevyo hawawezi kumruhusu aichezee katika ligi kuu ya
Tanzania Bara msimu ujao.
"Hatuna shida sana na Yondan,
lakini lazima taratibu zifuatwe, hivyo kama wanataka kuvunja mkataba
wake, lazima watulipe milioni 50," alisema Rage.
Yondan
amejiunga na Yanga baada ya kulipwa kitita cha sh. milioni 30 na pia
atakuwa akilipwa mshahara wa sh. milioni moja kwa mwezi.
Mara
baada ya Yanga kutangaza kumsajili mchezaji huyo, Simba iliwasilisha
malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai kuwa,
usajili huo ni batili.
Hata hivyo, TFF iliyatupilia mbali
malalamiko hayo ya Simba na kumruhusu Yondan kuichezea Yanga katika
michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni mjini Dar es
Salaam.
Reactions: |
MANJI AVUNJA KAMATI ZOTE ZA YANGA
Mwenyekiti
wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji ametangaza kuvunja kamati zote za klabu
hiyo zilizokuwepo katika uongozi uliopita chini ya mwenyekiti, Lloyd
Nchunga.
Manji alitangaza kuvunja kamati hizo leo wakati
akizungumza na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo katika makao makuu ya
Yanga, mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Uamuzi
huo wa Manji umekuja muda mfupi baada ya yeye na viongozi wenzake wapya
kula viapo vya uaminifu vya kuiongoza klabu hiyo mbele ya mdhamini mkuu
wa klabu hiyo, Mama Fatume Karume.
Mbali na Manji, viongozi wengine waliokula viapo hivyo ni makamu mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Hata
hivyo, Manji alisema kamati pekee itakayoendelea na majukumu yake ndani
ya Yanga ni ya uchaguzi inayoongozwa na Jaji John Mkwawa.
Manji
alisema anatarajia kuunda kamati zingine mpya baada ya kikao cha kamati
ya utendaji kinachotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Reactions: |
TENGA KUFUNGUA KOZI YA FIFA LEO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) anatarajia kufungua Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoanza kesho (Agosti 6 mwaka huu) Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo itakayokuwa na washiriki zaidi ya 30 itamalizika Agosti 11 mwaka huu na itaendeshwa na Wakufunzi kutoka FIFA na itafunguliwa saa 3 asubuhi. Wakufunzi hao ni Barry Rukoro anayetoka Namibia, Henry Tandau (Tanzania) na Senka Kanyenvu (Botswana).
Baadhi ya washiriki wa kozi hiyo ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.
Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe na Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba.
Wengine ni Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.
Reactions: |
MAMA KARUME AWAAPISHA VIONGOZI WAPYA YANGA
Mama Karume akiwasili makao makuu ya klabu ya Yanga na kupokewa na
mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, Francis Kifukwe (kulia). Kushoto ni
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu.
Mama Karume akiongozwa kuingia kwenye jengo la Yanga. Kulia ni
Mwenyekiti wa baraza la wazee, Jabir Katundu na kushoto ni mjumbe wa
kamati ya utendaji, Musa Katabalo.
Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuf Manji (kulia) akiteta jambo na mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, Francis Kifukwe.
Ni wakati wa kuomba dua. Hafla hiyo ilianza kwa viongozi na wanachama kusoma dua
Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa akifungua hafla ya uapishaji wa viongozi wapya
Yanga Oyee! Ndivyo anavyoelekea kusema Mama Karume kabla ya kuwaapisha viongozi wapya wa Yanga.
Tunatakiwa
kushikamana na kuwa wamoja. Ndivyo alivyosema Mama Karume wakati
akizungumza na viongozi wapya wa Yanga kabla ya kuwaapisha.
Mama Fatume Karume akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa huku Mzee Jabir Katundu akiwasikiliza.
Reactions: |
Saturday, August 4, 2012
DOGO JANJA ATAMANI KUKUTANA NA MADEE
Msanii
chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Janja amesema anatamani
kukutana na mlezi wake wa zamani, Madee wa kundi la Tip Top Connection.
Akihojiwa
katika kipindi cha Amplifier cha Clouds FM, Dogo Janja amesema tangu
aliporejea Dar es Salaam kutoka kwao Arusha, hajabahatika kukutana na
Madee.
Msanii huyo mahiri kwa kuchana amesema, mwanzoni
hakuwa akitaka kukutana na Madee kwa sababu ya hasira alizokuwa nazo,
lakini kwa wakati huu anatamani kumuona.
Madee ndiye
aliyevumbua kipaji cha Dogo Janja miaka minne iliyopita na kumuhamishia
mjini Dar es Salaam na kumtafutia shule katika sekondari ya Jitegemee.
Akiwa Tip Top, Dogo Janja alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na tungo zake na kupata ofa nyingi za kufanya maonyesho.
Hata
hivyo, uhusiano wa dogo huyo na Madee ulianza kuyumba na hatimaye
kukorofishana kabla ya Madee kuamua kumrejesha chalii huyo kwao Arusha
kwa madai kuwa, alikuwa hataki shule na alijikita zaidi katika anasa.
Lakini
Dogo Janja alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa, Madee alikuwa
akimtumia kupata pesa na kwamba kwa kipindi chote alichokuwa Tip Top
hajawahi kunufaika na kipaji chake zaidi ya kuambulia visenti vichache.
Kwa
sasa, Dogo Janja yupo katika kundi la Mtanashati linalomilikiwa na
mfanyabiashara, Ustaadh Juma Namusoma na tayari ameshaibuka na kibao
kipya.
Singo hiyo ni ya kwanza kuirekodi toka ameondoka
kwenye kundi la TipTop Connection June 13 2012 na imerekodiwa kwa Marco
Chali, MJ Records ambapo PNC amepewa shavu kwenye chorus. Ni singo
inayozungumzia maisha ya ukweli ya Dogo Janja.
Reactions: |
OKWI AMKARIBISHA NGASA SIMBA
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Okwi amemkaribisha
rasmi mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Mrisho Ngasa.
Okwi ametoa makaribisho hayo kwa Ngasa kupitia akaunti yake ya mtandao wa twitter leo.
Katika
maelekezo yake ya kumkaribisha Ngasa, Okwi ameandika 'Welcome to Simba,
Mrisho Ngasa, nguvu moja' , akiwa na maana 'Karibu Simba, Ngasa, nguvu
moja'.
Ngasa amesajiliwa na Simba akitokea Azam baada ya kulipwa kitita cha sh. milioni 30 pamoja na gari.
Mshambuliaji
huyo pia alikuwa akiwaniwa na klabu yake ya zamani ya Yanga, lakini
vibopa wake walichemsha baada ya kudai kuwa, hana thamani, ambayo Azam
ilikuwa ikitaka ilipwe ili imruhusu kuhama.
Reactions: |
YANGA YAMTAMBULISHA RASMI DIDIER KAVUMBANGU
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu akimkabidhi jezi namba 21
mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Didier Kavumbangu katika hafla
iliyofanyika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar
es Salaam. Yanga imemsajili Kavumbangu kutoka Atletico ya Burundi.
Reactions: |
Friday, August 3, 2012
HUU NDIO MKOKO MPYA WA NGASA ALIOPEWA NA SIMBA
Reactions: |
NGASA ALIVYOANZA MAZOEZI SIMBA LEO
Mrisho Ngasa akiteta jambo na Uhuru Selemani wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye ufukwe wa Coco Beach
Reactions: |
VIMBWANGA VYA OLIMPIKI
Lahaula! Mchezaji wa timu ya mpira wa mikono ya Angola akimkaba koo
mchezaji wa Uingereza wakati wa mechi ya michuano ya Olimpiki
Reactions: |
MAYWEATHER ATOKA JELA MWEZI MMOJA KABLA YA KUMALIZA KIFUNGO
Boxing superstar Floyd Mayweather walked free from a Las Vegas jail early on Friday morning after serving two months for battering his ex-girlfriend in front of their children.The undefeated five-division champion was greeted by 20 family and friends, including rapper 50 Cent, as he emerged from Clark County Detention Centre just after midnight.The 35-year-old remained silent as, in the darkness, he got into a blue Bentley sedan and drove himself away the three months jail time he was handed for a hair-pulling, arm-twisting attack on former lover Josie Harris as two of their three children watched.And he is now free to resume a boxing career his lawyers warned in court documents might be at risk because jail food and water did not meet his dietary needs.They also said his lack of exercise space in a cramped cell of fewer than 98sq ft threatened his health and fitness.
A lot has happened in Mayweather's world since he was jailed June 1. With no television in his solo cell, he could not see arch rival Manny Pacquiao lose his WBO welterweight title on June 9 to Timothy Bradley. Mayweather, who goes by the nickname 'Money', was also not around to celebrate last month when Forbes magazine named him the world's highest-paid athlete for 2011.
And he missed fiancee Shantel Jackson's private birthday bash last week at a Las Vegas steakhouse with friends.Las Vegas Review-Journal celebrity columnist Norm Clark noted that Mayweather sent diamonds. But Mayweather is now a free man, even if his next opponent is not immediately clear. Mayweather's manager Leonard Ellerbe did not respond this week to repeated messages from The Associated Press. Promoters for Mayweather's main rival, Philippine boxer Manny Pacquiao, are planning a fight for November 10 at the MGM Grand Garden arena in Las Vegas, Nevada Athletic Commission executive Keith Kizer said. Pacquiao's opponent has not been named but Mayweather was not believed to be on the list.
Pacquiao, who earned $62million in fights and endorsements last year, ranked second on the Forbes richest athletes list behind Mayweather and his $85million in fight earnings. To fight in Las Vegas, Mayweather will need a new license from the Nevada Athletic Commission, Kizer said yesterday.His last license, for the May 5 bout against Miguel Cotto, was for one fight only. If Mayweather applies, commission Chairman Raymond 'Skip' Avansino Jr could decide to grant approval administratively or summon Mayweather before the panel for a public hearing, Kizer said. Mayweather received about 30 days off his 90-day jail sentence for work time and good behaviour.Nevada state law allows inmates to receive up to 10 days off per month for co-operating with jailers and working or being willing to work. Las Vegas police administer the jail, and a department spokesman said Mayweather was not required to work and did not misbehave behind bars.
The plea deal allowed him to avoid trial on felony charges that could have gotten Mayweather up to 34 years in prison if he was convicted. Harris and the children have since moved to the Los Angeles area.As a high-profile inmate, police say Mayweather was kept separate for his protection from the other 3,200 inmates in the downtown Las Vegas facility. Las Vegas Justice of the Peace Melissa Saragosa rejected arguments that Mayweather's accommodations were cruel and unusual. The judge ruled June 13 that while Mayweather may not have liked the regimen, he had sufficient space and time for physical activity and the only reason he was not eating properly was because he was refusing to eat the meals he was given. The judge earlier gave Mayweather a break - allowing him to remain free long enough to make the Cinco de Mayo fight against Cotto at the MGM Grand Garden arena in Las Vegas.Mayweather won to run his record to 43-0 with 26 knockouts. Cotto lost for just the second time in 38 fights
Reactions: |
MICHUANO YA BANCABC ILIVYOZINDULIWA RASMI DAR
Mkurugenzi
Mtendaji wa Muunganiko wa Makampuni ya BancABC, Douglas Munatsi (kulia)
akimkabidhi Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania(TFF), Athuman Nyamlani kwa ajili ya mashindano ya BancABC SUP8R
wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano hayo na kuchezeshwa kwa Droo
maalum ya kupanga ratiba kamili ya michuano,uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Uongozi
wa BancABC na TFF wakiwa wameshikira Kombe kuashira Baraka njema na
kutakia mashindano mema ya BancABC SUP8R .Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa
TFF, Angetile Hoseah,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania(TFF), Athuman Nyamlani,Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC
Nchini,Boniphace Nyoni na Mkurugenzi Mtendaji wa Muunganiko wa Makampuni
ya BancABC, Douglas Munatsi.
Reactions: |
NGASA APEWA JEZI NAMBA 16 SIMBA
MCHEZAJI mpya wa Simba, Mrisho Ngassa, leo
amekabidhiwa jezi namba 16 atakayokuwa akiitumia
kwenye klabu yake msimu huu.
Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya
Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu
Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
Kaburu alisema Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo
mmoja na kwamba wapenzi wote wa Wekundu wa
Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake
mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.
"Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote
vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu.
Tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya
kumaliza muda wa mkopo wake kutoka Azam na ni imani
yetu kwamba ujio wa Ngasa utaimarisha zaidi timu kwani
yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa
Simba, Milovan Cirkovic, anawapenda," alisema.
Akizungumza katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi
kusajiliwa na Simba kwani ni sawa na historia kujirudia,
akikumbusha kwamba baba yake mzazi, Khlfan Ngassa,
aliwahi kuwa mchezaji wa klabu katika miaka ya 1990.
Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa
alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba katika
ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam ambako Simba
inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre
Richard na James Kisaka.

MAANDALIZI MKUTANO MKUU YAENDA VIZURI
MKUTANO Mkuu wa Wanachama Wote wa Simba
utafanyika Agosti tano mwaka huu katika Bwalo la Maofisa
wa Polisi Oysterbay kama ilivyopangwa.
Mipango yote kwa ajili ya mkutano huo muhimu kikatiba
imekamilika na klabu inawaomba wanachama wake wote
hai kuhudhuria mkutano huo muhimu.
Uongozi umepanga kutoa mabasi kwa ajili ya
kuwasafirisha wanachama wake kutoka katika maeneo
mbalimbali kwenda katika ukumbi wa mikutano.
Kutakuwa na mabasi matatu kwenye eneo la Shibam
Magomeni... Mabasi matatu Temeke mwisho na mabasi
matatu katika makao makuu ya Simba SC Mtaa wa
Msimbazi.
Pia klabu itapeleka mabasi mawili katika wilaya za
Mkuranga na Kibaha kwa ajili ya kuwaleta wanachama
wake walio katika mkoa wa Pwani kuhudhuria mkutano
huo.
Mwenyekiti wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage,
amewahakikishia wanachama wa Simba kwamba mkutano
huo utaendeshwa kisasa na usalama umehakikishwa kwa
asilimia 100 kwa vile eneo la mkutano liko chini ya Jeshi la
Polisi.
"Napenda kuwahakikishia wanachama wote wa Simba
kwamba mkutano huo utakuwa bora na wote watakaokuja
watafurahi na kujisikia fahari kuwa washabiki wa klabu ya
soka ya Simba.

"Kwa wale ambao wamepanga kuja kufanya
vurugu kwenye mkutano huo, klabu itaviachia vyombo vya
dola vifanye kazi yake," alisema.
vurugu kwenye mkutano huo, klabu itaviachia vyombo vya
dola vifanye kazi yake," alisema.
Reactions: |
BINGWA MICHUANO YA BANCABC SUPER 8 KUZOA MIL 40/-
Bingwa wa michuano ya BancABC Super 8 inayoanza
keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) katika miji ya Dar es
Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata sh. milioni
40.
Mshindi wa pili wa michuano hiyo atapata sh. milioni 20.
keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) katika miji ya Dar es
Salaam, Zanzibar, Mwanza na Arusha atapata sh. milioni
40.
Mshindi wa pili wa michuano hiyo atapata sh. milioni 20.
Pia timu mbili zitakazoishia hatua ya nusu fainali kila moja
itapata sh. milioni 15 wakati zilizobaki kila moja itapata
sh. milioni 5.
Timu zimepangwa katika makundi mawili ya A na B. Kundi
A lina timu za Simba (mabingwa wa Tanzania Bara),
Jamhuri, Zimamoto na Mtende zote za Zanzibar. Kundi B ni
Super Falcon (mabingwa wa Zanzibar), Azam, Mtibwa
Sugar na Polisi Morogoro zote za Tanzania Bara.
Mechi za ufunguzi keshokutwa (Agosti 5 mwaka huu) ni
Simba vs Jamhuri (Dar es Salaam), Zimamoto vs Mtende
(Mwanza), Mtibwa Sugar vs Polisi Morogoro (Arusha) na
Super Falcon vs Azam (Zanzibar).

Awali mashindano yalikuwa yaanze Agosti 4 mwaka huu
lakini yamesogezwa mbele kwa siku moja.
Hatua ya makundi itamalizika Agosti 12 mwaka huu. Mechi
za nusu fainali na fainali zote zitachezwa Dar es Salaam.
Nimeambatanisha ratiba.
Mdhamini bancABC atagharamia usafiri wa ndege kwa
timu zote kutoka kituo kimoja hadi kingine, malazi na jezi.
Yanga imejitokea kwenye mashindano hayo na nafasi yake
imechukuliwa na Mtibwa Sugar ambayo ilishika nafasi ya
nne kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

KOZI YA UONGOZI FIFA KUANZA AGOSTI 6
Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Msimbazi Center jijini
Dar es Salaam kuanzia Agosti 6-11 mwaka huu ikiwa na
washiriki 30.
Washiriki wa kozi hiyo itakayonedeshwa na wakufunzi
kutoka FIFA ni viongozi kutoka TFF, Chama cha Mpira wa
Miguu Zanzibar (ZFA), vyama vya mpira wa miguu vya
mikoa, klabu za Ligi Kuu na viongozi wa mpira wa miguu
wa wanawake.
Walioteuliwa kushiriki ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa
TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA Amani Makungu,
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi,
Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein
Mwamba na Eliud Mvella.
Wengine ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu
Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi),
Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
Makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya
Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri),
Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga
(Beatrice Mgaya) na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo
Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
Washiriki wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah,
Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa Habari,
Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio,
Jimmy Kabwe, Mkurugenzi wa Mashindano, Saad
Kawemba, Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay, Ofisa
wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina
Karuma (Mpira wa miguu wa wanawake) na nahodha wa
zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.

STARS KUIKABILI BOTSWANA AGOSTI 15
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Agosti 15 mwaka
huu itapambana na Botswana (Zebras) katika mchezo
maalumu wa Kalenda ya FIFA utakaofanyika jijini
Gaborone.
Tayari Kocha Kim Poulsen alishatangaza kikosi cha
wachezaji 21 kitakachoingia kambini Agosti 8 mwaka huu
tayari kwa mechi hiyo ya kirafiki ya kujipima nguvu.

LIGI DARAJA LA KWANZA SASA TIMU 24
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia msimu huu wa
2012/2013 itakuwa na timu 24 kutokana na mabadiliko ya
mfumo wa mashindano yaliyofanywa na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana Julai 29 mwaka huu
ambapo pamoja na mambo mengine ilifanya mabadiliko
ya mfumo wa mashindano ikiwemo FDL kuchezwa kwa
mtindo wa nyumbani na ugenini badala ya ule wa awali
wa vituo.
Kutokana na mabadiliko hayo, timu za FDL zitagawanywa
katika makundi mawili ya timu 12 kila moja kutokana na
ukaribu wa kanda na kucheza kwa mtindo wa nyumbani
na ugenini.
Timu ya kwanza kutoka kila kundi itapanda kucheza Ligi
Kuu msimu unaofuata wakati ya tatu itakayoungana na
hizo mbili itapatikana kwa mechi za nyumbani na ugenini
kwa timu zilizoshika nafasi ya pili katika kila kundi.
Ili kufikisha idadi ya timu 24 kwenye FDL, Kamati ya
Utendaji ya TFF kwa kuzingatia mapendekezo ya Kamati
ya Mashindano imeamua timu tatu za juu kwenye Ligi ya
Taifa kutoka vituo vyote vitatu vya ligi hiyo zimepanda
daraja.
Sasa timu 24 za FDL ni Ashanti United (Dar es Salaam),
Burkina Moro (Morogoro), Green Warriors (Dar es
Salaam), Kanembwa JKT (Kigoma), Kurugenzi Mafinga
(Iringa), Majimaji (Ruvuma), Mbeya City (Mbeya), Mkamba
Rangers (Morogoro), Mlale JKT (Ruvuma) na Morani
(Manyara).
Nyingine ni Moro United (Dar es Salaam), Mwadui
(Shinyanga), Ndanda (Mtwara), Pamba (Mwanza), Polisi
(Arusha), Polisi (Dodoma), Polisi (Iringa), Polisi (Mara),
Polisi (Tabora), Rhino Rangers (Tabora), Small Kids
(Rukwa), Tessema (Dar es Salaam), Transit Camp (Dar es
Salaam), Villa Squad (Dar es Salaam)
Timu nne zitashuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa. Timu hizo
ni mbili zilizoshika nafasi za mwisho kwa kila kundi. Timu
nne zitakazopanda kucheza FDL zitapatikana kwa mchujo
utakaohusisha mabingwa wa mikoa.
Kwa mfumo huo mpya wa mashindano, ligi za mikoa
zitakazosimamiwa na kuendeshwa na vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa zinatakiwa kuwa na timu zisizopungua 16
na zisizozidi 20. Ligi za mikoa pia zitachezwa mwaka
mzima kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini).
Ligi ya mkoa itashusha timu mbili na kupandisha nyingine
mbili kutoka ligi ya wilaya. Ligi za wilaya zitakazosimamiwa
na kuendeshwa na vyama vya mpira wa miguu vya wilaya
zinatakiwa kuwa na timu zisizopungua 10 na zisizozidi 20.
Kwa wilaya zenye timu zaidi ya 20, chama husika cha
mpira wa miguu kitapanga utaratibu wa kuzichuja kwa
mashindano ili kupata zile bora 20 zitakazocheza ligi rasmi
ya wilaya.
Mabingwa wa wilaya katika mkoa husika watacheza mechi
za kuchujana (play offs) ili kupata timu mbili
zitakazopanda daraja kucheza ligi ya mkoa husika.
Kutokana na mabadiliko hayo ya mfumo wa mashindano,
sasa madaraja rasmi ya ligi ni Ligi Kuu, Ligi Daraja la
Kwanza, Ligi ya Mkoa (Ligi Daraja la Tatu) na Ligi ya
Wilaya (Ligi Daraja la Nne).
TFF inasisitiza kuwa kwa mujibu wa kalenda yake ya
matukio, kipindi cha usajili wa wachezaji kwa madaraja
yote ni kimoja, na ligi zitachezwa kwa wakati mmoja.
Usajili wa hatua ya kwanza ni kuanzia Juni 15 hadi Agosti
10 mwaka huu wakati kipindi cha pili cha usajili ni Agosti
21 hadi Septemba 4 mwaka huu. Usajili wa dirisha dogo ni
Novemba 15 hadi Desemba 15 mwaka huu.
Ligi kwa madaraja yote zitaanza Septemba. Ligi Kuu
itaanza Septemba Mosi mwaka huu, Ligi Daraja la Kwanza
ni Septemba 15 mwaka huu, Ligi ya Mkoa na ile ya Wilaya
zenyewe zitaanza Septemba 8 mwaka huu.
Mechi za kufungua msimu kwa madaraja yote (Ngao ya
Jamii) ambazo kwa sasa zinakutanisha bingwa na makamu
bingwa zitachezwa Agosti 25 mwaka huu wakati michuano
ya Kombe la FA itaanzia wilayani Septemba 24 mwaka
huu.

Thursday, August 2, 2012
HATIMAYE NGASA AMWAGA WINO SIMBA, ALIPWA MIL 35/- NA GARI
HAKUNA
utata tena. Tamka Mrisho Khalfan Ngassa ni mchezaji halali wa Simba SC.
Mchana huu, klabu ya Simba imefanikiwa kumalizana na Ngassa na kusaini
naye mkataba wa miaka miwili, ambao umemfanya aondoke na zaidi ya Sh.
Milioni 35, Milioni 12 akipewa taslimu na nyingine akipewa gari.
Katika
mkataba huo wa Simba na Ngassa, mshambuliaji huyo atakuwa akilipwa Sh.
Milioni 2 mshahara kwa mwezi, Milioni 1 ipo kwenye mkataba na Milioni 1
atakuwa akiongezewa na mtu. Nani kakamilisha dili hili? Ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba SC, Hans Pop ndiye katoa fedha hizo na baada
ya kumsainisha na kumkabidhi haki yake, ili kumuondolea usumbufu
akambadilishia ‘chipu’ ya simu, ili akina Seif Magari wasimpate.
Jana
Simba ilimnunua Ngassa kutoka Azam kwa Sh. Milioni 25, lakini mchezaji
huyo wa zamani wa Yanga akagoma kwa sababu hakushirikishwa katika dili
hilo. Leo asubuhi Ngassa alizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria,
Maadili na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa kupinga kuuzwa kwake
katika klabu hiyo, akitokea Azam FC bila kuhusishwa.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY asubuhi ya leo, Ngassa alisema kwamba hajafanya
mazungumzo na Simba SC wala Azam FC juu ya uhamisho. “Mimi sijui
chochote, na sikatai kuhamishwa, kwa sababu mimi soka ni kazi yangu na
ninaweza kucheza popote, ila taratibu zifuatwe tu,”alisema.
Ngassa
alisema baada ya kuona mambo yanakwenda kinyume cha utaratibu, aakaamua
kulifikisha suala lake Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji
ili haki itendeke.
Kwa hatua hiyo, Simba imeamua
kuzungumza naye na kumaliza naye na sasa kijana ataanza mazoezi Simba
wiki ijayo, akitoka Mwanza anakokwenda leo kusalimia wazazi.
Azam
ilifikia uamuzi wa kumuuza Ngassa, baada ya mchezaji huyo iliyemsajili
kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, kubusu jezi ya Yanga baada ya
kufunga bao la pili katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC).
Na uamuzi huo, ni wa mzee Said Salim
Bakhresa mwenyewe, ambaye alikerwa na kitendo hicho akawaagiza wanawe,
Wakurugenzi wa bodi ya timu wamuuze mchezaji huyo popote, haraka
iwezekanavyo.Ngassa alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake
aliosaini na Azam FC, akitokea Yanga miaka miwili iliyoipita kwa dau la
Sh. Milioni 55, lakini wasiwasi unakuja kwamba, Ngassa ana mapenzi na
Yanga na kwa Simba kumsajili, kuna hatari yaliyotokea akiwa Azam,
yatajirudia hata akiwa kwa Wekundu wa Msimbazi.
Mapema
jana mchana, Stewart Hall, kocha Muingereza wa Azam FC jana alifukuzwa
katika klabu hiyo kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya
klabu hiyo, kumpanga Mrisho katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Habari ambazo
BIN ZUBEIRY ilizipata kutoka ndani ya Azam, zilisema kwamba kikao cha
jana cha pamoja baina ya Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC, Mwanasheria wa
kampuni na kocha Stewart kimeafiki kuvunja ndoa hiyo na sasa Azam FC
itakuwa chini ya kocha kutoka India, Vivek Nagul ambaye alikuwa
anafundisha timu ya vijana.
Habari zinasema kwamba, mapema
baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kagame, kati ya Azam na AS Vita ya
DRC, Stewart aliitwa na kuambiwa asimtumie tena Ngassa kwa kitendo cha
mchezaji huyo kwenda kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga, baada ya kufunga
bao la ushindi.
Lakini Stewart katika kikao hicho, kwanza
alimtetea Ngassa kutokana na kufunga bao la ushindi na kumuelezea kama
mchezaji muhimu kwake, lakini msimamo wa bodi ulikuwa ni asipangwe tena.
Katika
fainali, Stewart alimvalisha jezi Ngassa akamuanzishia benchi, lakini
kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali alimuingiza kipindi cha pili timu
ikiwa nyuma kwa 1-0 na mwisho wa mchezo ikashinda 2-1 yeye akifunga la
pili, dhidi ya Yanga pia alimuingiza timu ikiwa nyuma kwa 1-0.
Lakini
Ngassa alishindwa kurudia kile alichofanya kwenye mechi na AS Vita na
Yanga ikashinda 2-0.Kwa kutua Simba, Ngassa amefuata nyayo za baba yake
mzazi Khalfan Ngassa ambaye alichezea klabu hiyo kati ya 1990 hadi 1992.
CHANZO CHA HABARI; BIN ZUBEIRY
Reactions: |
Subscribe to:
Posts (Atom)
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI