Friday, August 9, 2013

SAKATA LA MFANYABIASHARA WA MADINI ALIYEPIGWA RISASI 6 JIJINI ARUSHA LEO MCHANA

KIJIWENIBONGO@
 
Habari zilizopatikana majira ya saa kumi kasoro robo alasiri ya leo zinafahamisha kuwa, Mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha na mmiliki wa hoteli amepigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Mijohoroni upande wa kulia (punde tu baada ya Boma Ng’ombe ukitokea Moshi kuelekea Arusha), mchana wa leo, alipokuwa ameitikia wito alioitiwa wa mazungumzo ya kibiashara ya madini.

Taarifa zinasema marehemu amepigwa risasi kati ya 6 - 12 katika paji la uso na maeneo mengine ya mwilini.

 
Mtu mmoja aliyewahi kufika kwenye eno la tukio baada ya kusikia milio ya risasi anasema alimkuta mtu mmoja wa fanani ya Kimasai ambaye alishuhudia tukio zima na kumsimulia kuwa aliona watu wanapiga risasi na kisha wakaondoka kwa pikipiki kuelekea porini huku akielekeza mkono kuonesha walikokimbilia.

Polisi wanaendelea na uchunguzi baada ya kuuchukua mwili wa marehemu kutoka kwenye eneo la tukio na kuupeleka hospitalini.

Mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Bomang’ombe.

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI