kijiweni bongo by paul koka
WATANZANIA leo wanaadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
WATANZANIA leo wanaadhimisha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Muungano huo ulisainiwa na waasisi wa mataifa hayo, hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika, hayati
Aman Abeid Karume aliyekuwa Rais kwa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ).
Zoezi la kutiliana saini ya kuuunganisha nchi hizo mbili na kuzaliwa
nchini moja Tanzania, ilifanyika tarehe 26 April mwaka 1964 kisiwani
Zanzibar na tangu hapo kukawa na Serikali mbili ndani ya Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya
Jamhuri wa Muungano.
Mpekuzi inawatakiwa watanzania wote popote
walipo duniani maadhimisho mema ya sherehe ya Muungano na Mungu
awasaidie waweze kudumisha Muungano wao na kuishi kwa amani na upendo
kama ilivyokuwa dhama ya waasisi wa jambo hilo.
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI