Picha zilizovuja za Dayna na Kala Jeremia wakiwa mkoani Singida
Hata hivyo, baada ya kufanikiwa
kuwapiga picha, alisambaza krip hiyo kwenye baadhi ya mitandao ambapo
ilianza kutoa hisia tofauti kwa wadau wa sanaa, wakiamini kuwa wawili
hao walikuwa wakifanya ngono katika chumba hicho.
Katika mtandao wa Youtube, watu wengi
walikuwa wakiporomosha matusi wakisema kuwa wasanii hao wanataka
kutumia ngono kama mbeleko yao ya kuwabeba kisanaa.
Dayna alipoulizwa juu ya tukio hilo
la kulala chumba kimoja na Kala Jeremia mkoani Singida, alisema kuwa
hawapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, ila Kitale anaandaa filamu ambayo
wao watakuwapo kwenye kazi hiyo ya aina yake.
“Ni kweli nasikia mengi mtaani na
wengine wanatukana wakisema eti sisi ni wahuni au tupo kwenye mapenzi,
ingawa ukweli ni kuwa tupo kwenye filamu zaidi.
“Mimi ni msanii, hivyo kuambiwa
nicheze filamu kwangu ni kwepesi zaidi, ndio maana naomba wadau na
mashabiki wangu waelewe kuwa sipo kwenye mapenzi na Kala,” alisema.
Hata hivyo Dayna hakuweza wazi ni
filamu gani anayocheza na Kala, huku akisema kuwa mwenye uwezo wa
kuizungumzia zaidi ni muandaaji mwenyewe Kitale.
kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI