Mh. Tundu Lissu Mbunge wa Jimbo la Singida Vijijini & Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Naibu Spika Ndugai jana aliamuru Tundu Lissu atolewe nje ya Bunge huku wabunge wa upinzani wakizomea na kuseama hatoki mtu.
Amri hiyo ilitokaea baada ya yeye
kuingilia kati mchango wa Mwigulu Nchemba aliyesema kwamba udini ni
jambo geni hapa nchini....
Tanzania imeongozwa na ccm tangu uhuru, na
marais wote wamekuwa wakitoka ccm, rais wa kwanza alikuwa mkristo, wa
pili muislam, wa tatu mkristo na wa nne ni muislam..akasema kama udini
ni jambo geni watanzania tujiulize limekujaje???? Kwanini sasa na sio
wakati huo???
Akasema katika kampeni za urais 2010
dr slaa akiwa katika kampeni mkoani singida alitumia viongozi wa dini
kufanya vikao vya kampeni badala ya kutumia wanachama wa chama
chake...na viongozi hao wapo tayari kutoa ushahidi...
Ndipo Tundu Lissu
aliposimama na kuomba mwongozo, spika akamwambia atulie kwa sababu Susan
Kiwanga tayari amepewa nafasi akalisemea hilo na muda ni mdogo Lissu
akang'ang'ania ndipo Naibu Spika akaamuru askari amtoe nje Lissu.
Pamoja na hayo Naibu spika
amewafungia vikao vitano kinyume na kanuni za Bunge Mh. Lema, Mh.
Mbilinyi. Mh. Kiwia, Mh. Msigwa, Mh. Wenje
kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI