Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina
la Bi Kidude amefariki dunia leo mchana huko Bububu
Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. Mwili wake
utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho.
Bi Kidude
alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa
nazi na hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata
mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102.
Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....
Mwaka
1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa
kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi Kidude pia aliwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni
BAADHI YA SHOW ALIZOWAHI KUFANYA JIJINI DAR ES SALAAM. HII ILIKUWA June 30, 2012
Shabiki akimtunza Bi Kidude
Mashabiki wakipozi juu ya jukwaa ili kupiga picha na Bi Kidude.
Bi Kidude akionyesha umahili wake wa kucheza.
Hii
ilikuwa usiku wa june 30 2011 katika ukumbi wa Equator uliopo Mtoni
kwa Azizi Ally ambapo kulifanyika onyesho la taarab, wanamuziki
mbalimbali wa taarabu waliudhuria akiwemo mwanamuziki mwalikwa toka
Zanzibar Bi Kidude.Baadhi ya bendi ambazo ziliudhuria onyesho hilo ni Five Star, TOT, East Africa Melod na Mashauzi Clasc
Baadhi ya picha enzi za uhai wake
Akitaniana na mtangazaji wa Clouds Tv, Sakina Lyoka
Akipiga ngoma
Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI