Watu
wanaosadikika kuwa ni wahuni wa kitechnolojia wameonekana kutenda
mambo yao katika Official website ya Daddy wa muziki wa rap Tanzania,
Proffesa Jay http://www.professorjaytz.com/ ambayo kwa mujibu
wake mwenyewe, site hii ilikuwa bado ipo katika matengenezo na kuna mtu
maalum ambaye alikuwa amemuasign kazi ya kuitengeneza.
Hivi ndivyo site ya msanii huyu inavyoonekana kwa sasa; |
Jay
mwenyewe ambaye hadi wakati tuliokuwa tunaongea naye alikuwa hafahamu
kuhusiana na kutokea kwa issue hii, amewaahidi mashabiki wake
kulifuatilia swala hili na kuhakikisha anaweka kila kitu katika mstari.
Rapa huyu mchana wa leo atakuwa akitoa Burudani pande za Chuo kikuu Cha Dar es Salaam katika Kongamano maarufu la Kigoda Cha Mwalimu Nyerere kwa mwaka huu, Kongamano ambalo limeanza jana na linatarajiwa kuisha siku ya kesho likiwa na kauli mbiu 'Maendeleo ni Mapambano ya Ukombozi'.
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI