kijiweni bongo by paul koka
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Seleman Rashid wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Anna Mallac (Chadema) aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuwawajibisha wageni wanaowazalisha wanawake na kuwatelekeza ili kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na kupunguza wimbi la watoto wa mitaani.
Dk Seif Seleman Rashid. |
Mama wa mtoto aliyetelekezwa anawajibika kuwasilisha shauri la matunzo ya mtoto katika vyombo vya sheria.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Seleman Rashid wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Anna Mallac (Chadema) aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuwawajibisha wageni wanaowazalisha wanawake na kuwatelekeza ili kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na kupunguza wimbi la watoto wa mitaani.
Naibu
Waziri alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009,
kifungu cha 43, mama wa mtoto aliyetelekezwa anawajibika kuwasilisha
shauri la matunzo ya mtoto katika vyombo vya sheria.
Alifafanua
“Wizara yangu kama msimamizi na mtekelezaji mkuu wa sheria hii baada ya
kupokea mashauri ya aina hiyo hufanya mawasiliano na Wakala wa Kimataifa
wa Huduma za Jamii ili kuweza kufanya uchunguzi na ufuatiliaji katika
upande wa mlalamikiwa ambaye ndiye anayedhaniwa kuwa baba wa mtoto”.
Baada
ya uchunguzi huo inapothibitishwa pasipo shaka kuwa mlalamikiwa ndiye
baba halisi wa mtoto husika , taratibu za malezi , matunzo na ulinzi wa
mtoto huyo hufanywa kwa kutumia ofisi za balozi za nchi husika.
Mbunge
huyo wa Viti Maalumu, ambaye alisimama tena kwa swali la nyongeza
alilielezea Bunge kuwa raia wa China na Uingereza wanaofanya shughuli za
ukandarasi wa ujenzi wa barabara vijijini na kwenye machimbo
wamewazalisha wanawake vijijini watoto na kisha kuwatelekeza na kurudi
katika nchi zao.
“Wanawake hao wanahangaika na watoto wao weupe
wamechakaa utawaona wameshikilia muhindi huku baba zao Wachina na
Waingereza waliowazalisha wamerudi kwao je, Serikali haioni sasa itoe
elimu kwa wanawake hao ili waweze kwenda kupata haki zao,” alihoji
Mbunge huyo.
Hata hivyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Sophia Simba alimtaka mbunge huyo na wananchi wengine kutumia
njia za uzazi wa mpango ili kuzuia mimba zisizohitajika.
Katika
kuelezea suala la ulinzi Naibu Waziri Afya na Ustawi wa Jamii alisema
katika kuhakikisha haki za watoto walio katika mazingira hatarishi
hususan watoto waliotelekezwa, wanaonyanyaswa na kufanyiwa vitendo vya
ukatili zinalindwa, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Halmashauri na
wadau wa maendeleo imeanzisha programu ya ulinzi na usalama wa mtoto
ambapo mifumo ya ulinzi na usalama wa watoto imeimarishwa kwa kuundwa
timu za ulinzi katika ngazi ya halmashauri, kata na vijiji na mitaa.
“Hadi
sasa mifumo ya ulinzi na usalama imeanzishwa katika halmashauri za Hai,
Magu, Kasulu, Temeke, Nyamagana, Ilemela, Kinondoni, Ilala, Musoma na
Bukoba. Timu hizo hujumuisha wataalamu mbalimbali wanaohusika na ulinzi
wa watoto wakiwemo maofisa ustawi wa jamii,” alisema.
Alisema katika
mwaka wa fedha 2013/2014 programu ya ulinzi na usalama itasambazwa
katika halmashauri 25 hivyo kupitia programu hiyo matukio ya
unyanyasaji, utelekezaji na ukatili kwa watoto utazuiwa na
kushughulikiwa ipasavyo.
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI