MUSA TESHA BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI
------------------
Kada
maarufu wa CHADEMA Shinyanga mjini,Bwana Oscar Kaijage,Jumamosi
alikamatwa na askari polisi na kuzuiwa kituo cha kati na jana Jumatatu
alisafirishwa kwenda Tabora na kukabidhiwa kwa askari wa huko.
Sababu kuu ya kukamatwa,ni kuhusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali Bwana Musa Tesha 9 Sept,2011 huko Igunga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbunge ambapo mgombea wa CCM bwana Peter Kafumu alimshinda mgombea wa CHADEMA bwana Joseph Kashinde.
Bwana Oscar alifuatwa dukani kwake stand ya mabasi ya Shinyanga mjini mnamo saa 9 mchana na askari nane ambao hawakuvaa sare.
Baada ya mazungumzo ya muda mfupi askari hao waliwaomba majirani wa duka hilo wasogee ili wawe mashuhuda wakati wanampekua.
Hata hivyo,polisi hao hawakukuta kitu chochote walichokihitaji na kuamua kuondoka naye kwenda kumpekua nyumbani kwake ambako nako pia hawakuambulia kitu.
Taarifa iliyopatikana jana mchana kutoka ofisi ya RPC shinyanga ni kuwa Oscar amepelekwa Tabora kwenda kufunguliwa mashitaka.
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI