Mshukiwa
wa mwisho katika utegaji wa mabomu yaliyowauwa watu 3 na kuwajeruhi
wengine zaidi ya 180 katika mbio za Marathon za Boston amekamatwa akiwa
ndani ya boti. Polisi imesema kuwa amepelekwa hospitali akiwa mahututi.
Kukamatwa
kwa mtu huyo Dzhokhar Tsarnaev, mwenye umri wa miaka 19 kumehitimisha
operesheni kubwa ya siku nne, na kumekuja siku moja baada ya shirika la
upelelezi la Marekani FBI kuchapisha picha za washukiwa hao.
Mshukiwa mwingine, Tamerlan Tsarnaev mwenye umri wa miaka 26 na ambaye ni kaka wa Dzhokhar, aliuawa jana Ijumaa katika majibizano ya risasi na polisi.
Mshukiwa mwingine, Tamerlan Tsarnaev mwenye umri wa miaka 26 na ambaye ni kaka wa Dzhokhar, aliuawa jana Ijumaa katika majibizano ya risasi na polisi.
Tamerlan Tsarnaev (Kushoto) na mdogo wake Dzhokhar
Umati
wa watu katika mji wa Boston ulishangilia kwa shangwe baada ya kuibuka
kwa ripoti ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo. Shughuli zote katika mji huo
zilikuwa zimesimamishwa wakati operesheni ya kuwasaka vijana hao
ilipokuwa ikiendelea.
Bado yapo maswali yasio na majibu
Akizungumza
muda mfupi baada ya kukamatwa kwa Dzhokhar Tsarnaev, rais wa Marekani
Barack Obama alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ilikuwa hatua muhimu
katika mkasa unaohusu miripuko ya Boston.
Hata
hivyo, Obama alisema kuwa bado yanabakia maswali yasio na majibu,
ambayo ni pamoja na sababu iliyowafanya vijana hao kufanya mashambulizi,
na ikiwa walikuwa na msaada katika uhalifu wao.
''Tutatathmini
kilichotokea, na tutachunguza kama magaidi hawa walikuwa na washirika,
na tutafanya chochote kinachohitajika kuhakikisha usalama wa watu'',
alisema rais Obama.
Mripuko kwenye mbio za Marathon za Boston iliuwa watu 3 na kujeruhi zaidi ya 180
Polisi
mjini Boston wamesema kuwa watu wengine watatu wamekamatwa na
wanahojiwa kwenye nyumba aliyoishi Dzhokhar Tsarnaev karibu na chuo
kikuu cha Massachusetts.
Polisi
wamesema walikuwa wakianza kukata tamaa katika operesheni yao, hadi
pale walipopigiwa simu na raia ambaye ameiona damu kwenye boti yake, na
kumkuta mshukiwa ndani ya boti hiyo akiwa ametokwa na damu nyingi.
Hisia kali dhidi ya Marekani
Watuhumiwa
hao wametambuliwa kuwa ni jamii ya Chechen kutoka kusini mwa Urusi,
ambao inaaminiwa wamekuwa wakiishi Marekani kwa muda wa miaka 10. Jimbo
la Chechnya limeshuhudia vita viwili vikubwa tangu mwaka 1994, baina ya
Urusi na wapiganaji wanaotaka kujitenga kwa jimbo hilo.
Kaka
mkubwa Tamerlan anasemakana alikuwa na maoni makali dhidi ya Marekani,
akiishutumu nchi hiyo kutumia Biblia kama kisingizio kuzivamia nchi
nyingine.
Kabla
ya kukamatwa kwa mdogo wake mji wa Boston ulikuwa umepooza, baada ya
utawala kufunga barabara zote na kuwashauri wenye biashara kuzifunga.
Hali kadhalika wakazi milioni moja wa mji huo na vitongoji vyake
walikuwa wameombwa kubakia ndani ya nyumba zao, na kufungua mlango tu
kwa maafisa wa polisi waliovalia sare.
kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI