Mamia
ya watetezi wa haki za mashoga nchini New Zealand wamefurahia hatua ya
uamuzi wa bunge la nchi hiyo wa kuhalalisha ndoa za jinsia sawa.
New Zealand imekuwa nchi ya 13 duniani na ya kwanza katika eneo la Asia-Pasifik kuchukua hatua hiyo.
Wabunge 77 walipiga kura kuunga mkono mswada huo na 44 waliupinga baada ya kuwasilishwa bungeni kwa mara ya tatu na ya mwisho.
Wananchi
waliokuwa wamekaa katika sehemu ya wageni bungeni, pamoja na wabunge
wenyewe walianza kuimba mara baada ya uamuzi kutangazwa.
Hata hivyo watu wengi nchini New Zealand wanapinga ndoa za jinsia moja.
Kundi
la wapiga debe-linaloitwa “Family First” mwaka jana liliwasilisha hati
ya malalamiko bungeni, iliyotiwa saini na watu nusu milioni kupinga
mswada juu ya kuhalalisha ndoa za mashoga
kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI