Wednesday, April 24, 2013

BINTI ANUSURIKA KUBAKWA BAADA YA KUKATIZA MITAA YA SINZA AKIWA AMEVAA KIMINI

kijiweni bongo by paul koka

 


Wanawake ambao majina yao hayakupatikana, wakazi wa Sinza, Dar es Salaam wamekumbana na sekeseke  la aina yake la ubakaji kisa kikiwa ni uvaaji wa vimini ambao kwa sasa umeshika kasi kila kona Bongo...

Mwanahabari wetu mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa manane, alinyetishiwa tukio la wanawake watatu kuvamiwa na midume na kufanyiwa kitu mbaya baada ya  kuchaniwa vimini vyao maeneo ya Barabara ya Shekilango, Dar kabla ya kuokolewa na wasamaria wema.

Wasichana hao, wakiwa wamejipodoa vilivyo na kutinga vimini vilivyoonesha sawia maungo yao nyeti bila ‘makufuli’, walijikuta  katika hali hiyo mbaya baada ya kurushiana maneno na vijana hao wahuni hivyo wakaonja joto ya jiwe.

Warembo hao ambao walikuwa wakitokea Sinza kuelekea Manzese, Dar walivamiwa na vijana hao ambao wengi wao ni waendesha  pikipiki maarufu kama bodaboda,  walipokaribia Makutano ya Barabara ya Shekilango na Morogoro, Dar.

“Kila siku wanapita hapa wakiwa nusu utupu, sasa leo tumewakomesha, serikali inatangaza Ukimwi ni hatari, wao hawajali,  wanatutia majaribuni,” alisikika akisema mwendesha bodaboda mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliowavamia wasichana
hao.

Mwendesha bodaboda mwingine alimwambia  mwandishi wetu  kuwa waliwaeleza wasichana hao kuacha tabia ya kutembea nusu utupu kwani ni hatari kwa maisha yao na ni kinyume cha maadili ya Watanzania lakini walijifanya jeuri ndiyo maana wakawaadabisha.
Aliweka wazi kuwa baada ya kuelezwa hivyo akina dada hao hawakufurahishwa na maneno hayo na badala yake
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali iliyowafanya wapandwe na hasira.

“Madereva wale baada ya kusikia wakitukanwa waliwavamia wasichana hao na kuanza kuwachania nguo kwa maelezo kwamba badala ya kuwa nusu utupu, ni vema wakakaa uchi wa mnyama kabisa.

“Warembo wawili walifanikiwa kutimua mbio licha ya kuchaniwa vimini vyao lakini mmoja aliyekuwa na ‘mdomo mchafu’ 

“Shukrani ziwaendee wasamaria wema waliomukoa kwa sababu kwa vyovyote lazima angebakwa kwani alikuwa  ameshachaniwachaniwa nguo na ku... ,” alisema shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa binti huyo alifanyiwa kitu mbaya kwa kushikwa sehemu nyeti kabla ya wale wenzake waliokimbia kurudi wakiwa kwenye Bajaj na mabaunsa wao kisha kutokomea na mwenzao aliyekuwa amehenyeshwa vya kutosha na wanaume
hao.

“Wale wasichana wawili walirudi wakiwa na Bajaj na mabaunsa, wakasaidiwa na raia wema ndipo wakafanikiwa kumuokoa  mwenzao na kutokomea naye kusikojulikana,” alisema shuhuda huyo.

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI