Friday, March 29, 2013

MACHANGUDOA WAJIUZA MBELE YA NYUMBA YA WAZIRI MKUU....


Issa Mnally na Richard Bukos-GPL
KWELI ni aibu kwa taifa kama la Tanzania, lenye ulinzi uliotimia lakini ni ajabu sana kuwaona wanawake wanaoishi mjini kwa kutegemea biashara haramu ya kuuza miili ‘machangudoa’ wamefikia kuifanya jirani kabisa na makazi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda.

Wiki iliyopita, waandishi  wetu  waliwanasa machangudoa hao wakiwa wanazurura kwenye Barabara ya Kenyatta inayopita mbele ya makazi ya waziri mkuu takriban mita 80 kutoka barabarani kwa lengo la kujiuza.


Ili kulijua hilo kwa undani, waandshi wetu walijifanya wateja kabla ya kuwapiga picha ili kuweza kuzungumza nao mawili matatu kuhusu kuwepo eneo hilo lenye heshima zake.
Mmoja wa ‘wauza sukari’ hao aliyejitambulisha kwa jina la Hawa, mkazi wa Kinondoni, alikiri yeye na wenzake kufanya biashara hiyo kwenye eneo hilo.


“Ni kweli mimi na wenzangu tunapiga kambi eneo hili, huwa ikifika usiku tunaanzia kule Coco halafu tunakuja hadi huku, lakini mbona maswali mengi, unataka tufanye biashara kama vipi sepa,” alisema changu huyo akianza kupandisha jazba.


Kikubwa walichokiongea machangu hao walisema barabara hiyo yote hupitwa na viongozi wakubwa na wafanyabishara ambao baadhi yao ni wateja wao wakubwa. Wakasema hawamwamini sana mteja anayekwenda na Bajaj au Bodaboda kwa vile wanasumbua kutafuta eneo la kufanyia ngono.


“Wateja wetu wengi ni wale tunaomalizana ndani ya gari, hawa wa Bajaj na Bodaboda wengi wanataka kwenye majani, ni rahisi kukamatwa na polisi wa doria,”
alisema changudoa mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Suzy lakini hakuwa tayari kutaja yaliko makazi yake.

Inakuwaje wauza miili hao watanue eneo ambalo kimazingira linapitiwa na viongozi mbalimbali wazito kama vile mabalozi wa nje waliopo Tanzania, mawaziri, akiwemo waziri mkuu mwenyewe ambaye ni jirani kabisa na makazi yake?

Yapo madai kwamba, askari wanaovalia mavazi ya kiraia ambao wanapaswa kuhakikisha usalama wa eneo lote la Coco Beach wanakaushia matendo hayo kwa kile kinachodaiwa wanapozwa na kitu kidogo.


“Askari wapo, lakini sema baadhi yao wanatufahamu, kwa hiyo ikitokea na sisi mambo yetu yamekaa vizuri tunachekiana,” alisema Suzy.
kijiweni bongo by paul koka

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI