Taarifa imetufikia kwamba utafiti wa haraka uliofanywa na umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT umeonyesha kwamba kwa Dar es salaam pekee, ni zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania haitazami channel za TV za nyumbani toka kuzimwa kwa mitambo ya analog ndio maana umoja huo bado umeendelea na msimamo wa kuitaka serikali kuangalia upya uwezekano wa kurudisha matangazo ya analog kwanza.
Haya ni maelezo ya mwenyekiti wa MOAT Reginald Mengi: “Watanzania wapewe muda kujiandaa ili kutoka analog kwenda digital ifanyike vizuri na kwa mafanikio makubwa, pendekezo letu lilikua ni kwamba analog na digital ziende sambamba mpaka tufike mahali tuone kwamba watu wengi kama sio wote wana vyombo vya kuwawezesha kwenda digital, hilo lifanyike kabla ya tarehe 17 june 2015 ambayo ndio siku ya mwisho ya kutumia analog” kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI