Home »
habari za kitaifa
,
JOKATE MWEGELO
» "SINA KINYONGO JUU YA PENZI LA DIAMOND NA PENNY"...JOKATE
BAADA
ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa
‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi
kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja
kama kweli wamependana na kuridhiana.
Jokate
ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa
anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano
wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa
dhati.
“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.
Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI