-------------
Baada
ya kuingia kwenye headlines na kukanusha kwamba hajafanyiwa opareshen
ya kuondoa nyama zilizozidi tumboni kwake, mwigizaji Mnigeria Omotola
Jalade ambae amewahi kuja bongo kuzindua movie mpya ya Wema Sepetu,
ameingia tena kwenye headlines.
Sasa
hivi amehusishwa na taarifa za kuaminika kwamba amekua akimpiga mumewe
aitwae Mathew Ekeinde, na hiyo hutokea mara kwa mara pale wanapokosana.
Stori
inaendelea kutiririsha kwamba pamoja na tabia hiyo aliyonayo Omotola,
Ekeinde amekua mvulivu na mwenye busara na amejizuia sana manake
hajawahi kumpiga hata siku moja kwa sababu anampenda sana.
Omotola
kweli anahulka ya kibabe, nakumbuka wakati alipokuja bongo nilipata
nafasi ya kuingia kwenye chumba chake alichokua analala, nilikwenda
kumfanyia interview… nilishuhudia jinsi alivyokua akimuendesha Cameraman
wake kibabe, pia alimzodoa kibabe mbele ya watu kijana mmoja ambae
alimkubalia kupiga picha lakini kijana akamshika Omotola kiunoni, ghafla
mwigizaji huyo akabadilika na kumuwakia kwamba asimfananishe na madem
wa saizi yake, hatakiwi kumshika hivyo.
Millard.
kijiweni bongo by paul koka
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI