Friday, October 19, 2012

WANANCHI WAVAMIA MASHAMBA YANAYO MILIKIWA NA

Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.

(PICHA,  HABARI  NA JOSHUA MWAKABUNGU WA FULLSHANGWE SUMBAWANGA)
……………………………………………….
Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha 
Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya
Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa 
baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.
 
Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara 
iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela
Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma 
kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.
 
Kamnda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia
watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani

Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.
Moja ya makambi yaliyoteketea kwa kuunguzwa na moto wakati wananchi hao walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba hilo.

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI