Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma kushoto na Salim Tawfik wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujitoa kwao siku ya leo katika kesi hiyo kutokana na usumbufu wanaofanyiwa wateja wao kuhangaishwa na kukosa kupelekwa Mahakama ya Kwerekwe kwa muda muafaka
Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake sita walioletwa Mahakama Kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali za watu zenye thamani ya Sh. 50 milioni na kufanya vurugu za makusudi za kuhatarisha amani katika nchi.
Baadhi ya Askari wa kutuliza fujo wakiwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga kwa lengo la kutuliza amani Mahakamani hapo. Viongozi hao wote wamerudishwa Rumande.
Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
No comments:
Post a Comment
KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI