Monday, October 22, 2012

TAHAHARI KUHUSU MABOMU 30 KUTOKA MALAWI

Kuna taarifa kwenye mitandao ya simu inayoendelea kutolewa kwenye message za simu kwamba  kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye uzito usiopungua tani 100 na kuwataka wananchi katika mikoa ya Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa waangalifu. 
Taarifa hiyo imetaka wenye wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige simu 0756000042. Taarifa hiyo imedai kwamba imetolewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Tunapenda kutoa taarifa kwamba taarifa hizo siyo za kweli na lengo lake  haliwezi kuwa zuri kwa Watanzania. 


 Wananchi wanashauriwa kutotuma taarifa zozote kwenye namba hiyo ama kuziamini taarifa za aina hiyo.
kijiwenibongo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI