Thursday, October 25, 2012

Azifunga Kufuli Sehemu za Siri za Mkewe ili Asitoke Nje ya Ndoa


NewsImages/6650638.jpg

Kwa miaka minne iliyopita, Sohanlal Chouhan, mwanaume mwenye umri wa miaka 38 wa Indore, India alikuwa akiufunga kwa kufuli uke wa mkewe kila alipokuwa akienda kazini ili kumlinda mkewe asitoke nje ya ndoa.

Kwa mujibu wa polisi, uchunguzi wa polisi ulianzishwa mwezi julai mwaka huu wakati mke wa Sohanlal aliyejulikana kwa jina la Sitabai Chouhan, alipowahishwa hospitali ili kuokoa maisha yake kufuatia jaribio lake la kujiua kwa kunywa sumu ya panya.

Madaktari walikuwa wanajiandaa kuingiza mrija kwenye sehemu za siri za Sitabai ili kusaidia kunyonya sumu ya panya toka kwenye mwili wake wakati walipogundua kuwa uke wake ulikuwa umefungwa kwa kufuli.

Iligundulika kuwa Sohanlal Chouhan alianza kuliweka kufuli kwenye sehemu za siri za mkewe miaka minne iliyopita kwa kuhofia mkewe angemsaliti na kutoka nje ya ndoa.

Wapelelezi walisema kuwa Sohanlal alifanikisha zoezi lake la kuweka kufuli kwenye uke wa mkewe kwa kumlewesha mkewe na kisha kutumia sindano kutoboa matundu mawili kwenye kuta mbili za uke.

Kufuli dogo lilipitishwa kwenye matundu hayo na lilikuwa likifungwa kwa ufunguo kila siku asubuhi wakati Sohanlal alipokuwa akitoka kuelekea kazini.

Kwa kuwa siku zote Sohanlal alikuwa akiondoka na funguo za kufuli hilo, madaktari walishindwa kumpatia tiba ya kutosha hadi mumewe alipolazimishwa atoe funguo ili kulifungua kufuli hilo.

Polisi walisema kuwa Sohanlal alikuwa ameificha funguo ya kufuli hilo kwenye soksi wakati alipokamatwa na kutiwa mbaroni.

Sohanlal amekiri kosa lake akidai kuwa alilazimika kufanya hivyo kwakuwa wanawake wengi kwenye familia yake walikuwa si waaminifu kwenye ndoa zao.

Sitabai ambaye amefanikiwa kuzaa watoto watano na Sohanlal ilidaiwa kuwa aliamua kujiua baada ya kugundua kuwa Sohanlal alikuwa akiisaliti ndoa yao.

Sohanlal alitupwa rumande na kufunguliwa mashtaka ya kufanya shambulio la kudhuru mwili.

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI