Sunday, August 18, 2013

MTANZANIA AKAMATWA HONG KONG NA MADAWA YA KULEVYA YAKIWA NDANI YA MASHINE

KIJIWENIBONGO@
 
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.

Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.

Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.

Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo  na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini. 

  

 
 

No comments:

Post a Comment

KIJIWENI BONGO HAITAUSIKA NA MAONI YANAYOWEKWA NA WASOMAJI